Kila ndoa inachangamoto zake na
maana halisi ya ndoa ni ule uwezo wa wanandoa kuvumiliana katika
changamoto hizo. Kuna changamoto za kimungu ambazo wanandoa hawawezi
kuziepuka lakini kuna zile za kiuanadamua mbazo nyingi ni za kimakusudi
na mtu huamua tu kuwa hivyo. Katika kuangalia ndoa leo nimeona nichambue
aina kumi za waume ambao wake zao wanakereka kuwa nao;
(1) Wanaojione Kama Wafalume (King Husband);
HIi ni aina ya wanaume ambao hutaka kusujudiwa kama wafalme na hupenda
kuwafanya wake zao kuwa kama watumwa. Hawafanyi chochote ndani ya nyumba
kazi yao ni kutumatuma hata kama mke anaumwa atapaswa kuamka na kupika,
wanataka waheshimiwe wao tu na mwanamke akikosea kidogo ni maneno au
kipigo. Mwanamke hana kauli ndani na mume akiingia nyumbani ni kama bosi
anavyoingia ofisini, wote kimya hakuna hata kuongea.
(2) Wanaume Wanaojihisi Bado Hawajaoa (Bachelor Husband);
Hii ni aina ya wanaume ambao hawawashirikishi wake zao kwa chochote.
Hufanya mambo kama vile bado hawajaoa, hutumia muda wao mwingi na
marafiki zao wakifanya mambo ambayo mke hata hayajui mke anaweza
kustukizia tu mume kanunua gari bila kumshirikisha na mume haonyeshi
hata kujali kuweza kumshirikisha. Hajali kama ana mke na mda mwingi
huutumia akiwa na marafiki kufanya mambo yasiyo na msingi ambayo hayana
mnanufaa yoyote katika ndoa yake.
(3) Wanaume Wenye Gubu (Acidic Husband);
Hawa hukasirika kila mara tena bila kua na sababu ya misngi, mambo
hayaishi, kosa la mwaka juzi anaweza kukukasirikia leo. Wamemuudhi
kazini hataki kusemeshwa na mnanuniwa nyinyi, mwanamke akiomba hela ya
chakula ni shida ni kununa kutwa nzima, wanahasira na nirahisi kumpiga
mke.
(4) Mume Wa Kila Mtu (Genarel Husband);
Hawa wanajifanya wasamaria wema, wanajali kila mwanamke, wanajali
marafiki wakike wa mke na wakwao kuliko wanavyowajali wake zao. Mke
anaweza kuwa na shida akasema hana hela lakini rafiki akampa. Wana
marafiki wengi wakike na mara nyingi huwa hawaachani kabisa na ma X wao,
wakiwalalamikia wanawasaidia kuliko hata wanavyowasidia wake zao wakati
wakiwa na shida.
(5) Wanaume Wanaojifanya Wagumu (Dry Husband);
Hawa wanajifanya wagumu sana, hawana yale mambo ya kimahaba na wao
hujua kuwa ndoa ni kuleta chakula tu na kushughulika kitandani. Hakuna
kuongea na hawajali hata hisia za mke, mke akiongea kwao wala hawajali
wanajifanya ni vidume sana na wanaona mambo kama vizawadi, kupiga simu,
kutuma sms, kusema nakupenda, kununua maua ni mambo ya kike, yaani
hawaonyeshi juhudi yoyote kuwafurahisha wekea zao.
(6) Wanaume Wanaopenda Kutumia Wake Zao (Panadol Husband);
Hawa huwa wanaume pale tu wanapokuwa na shida, wanakuwa na wake wazuri
wanaowajali lakini wao wala hawajali. Wanapomhitaji mwanamke, wanapotaka
mwanamke awafanyie kitu flani basi huja na maneno mazuri na hata kuleta
vizawadi, wanajua udhauifu wa wake zao na huutumia kuwalaghai
kuwatimizia mahitaji yao lakini wanapotimiziwa tu basi husahau hata kama
wanawake, hawajali tena.
(7) Wanaume Ambao Hawataki Kukua (Baby Husband);
Bado wanatabia za kitoto, hawawezi kufanya maamuzi yao wenyewe mpaka
kuuliza kwa ndugu zao, mtu kaoa lakini kila siku humpigia simu Mama yake
kuuliza hiki na kile. Yaani wakiongea kitu na mke nilazima aulize ndugu
kwanza ndiyo kipitishwa na mke akifanya kosaa kidogo kazi
nikulinganisha mke na ndugu zake, mbona flani alifanya hivi, flani
anaweza fanya zaidi na mambo kama hayo. Kwakifupi hawawezi kufanya
maamuzi na mkewe, ndugu zake hasa Mama yake anakuwa kama shemeu ya ndoa.
(8) Mume Mtalii (Visiting Husband);
Hawa wanakuja nyumbani kama wageni vile, mume ataihudumia familia yake
kwa kila kitu lakini hawezi kuipa muda wake. Akirudi mke na watoto
wamelala ni kugonga na hana sababu za msingi za kuchelewa, hata mwisho
wawiki hupenda kutumia na marafiki au ndugu lakini si na mke. Hakuna
kitu cha pamoja ambacho anafanya na mkewe au watoto wake, kila akiingia
tu anakua na safari ya kutoka yaani hata atoke akakae nnje tu lakini si
kukaa na mke au watoto.
(9) Wanaume Wanaofuatilia Kila Kitu (Stalking Husband);
Hii ni aina ya wanaume ambao hufuatilia kila kitu, huchunguza kila kitu
mwanamke anachofanya na hawampi pumzi. Akienda sehemu atachunguza
anaenda na nani na alikutana na nani, huwa na wivu wa ajabu ajabu na
kila saa huhisi wake zao ni wasaliti. Kila mtu mwanamke anayeongea naye
wa jinsia tofauti huhisi ni mchepuko na hata marafiki wa mke wakike pia
huhisi wanamkuwadia, kwakifupi hampi pumzi mwanamke.
(10) Mwanaume Mbahili (Miserly Husband);
Huyu anaweza kuwa na hela lakini mbahili ajabu. Akimpa mwanamke hela
atafuatilia matumizi yake mpaka senti ya mwisho, anafuatilia mpaka mambo
ya jikoni. Sukari ikiisha naataka ajue iliisha ishaje na kila mara
huhisi mke anamuibia hela labda akajenge kwao, huwa msumbufu sana na
mgumu kutoa hela. Mwanamke akifikiria mchakato wa kuomba hela kwa mume
hukata tamaa na wakati mwingine kuamua tu kukaa kimya na matatizo yake.
Hiyo nji baadhi tu ya aina ya
wanaume ambao wanawake wengi wasingependa kuwa nao. Kama mwanaume upo
hivyo jua mke wako hafurahii na anavumilia tu. Ndoa ni furaha amua
kubadilika na usimfanye mke wako kuishi na wewe kwa kujilzaimisha. Kama
ni mume jiulize uko namba ngapi hapo na kama ni mke mezea namba ya mumeo
na jua hauko peke yako.
No comments:
Post a Comment