“Miaka kumi iliyopita nilikuwa
katika kipindi ambacho wasichana wengi wapo kwa sasa…” Anaongea Dada
Anna. Nilikuwa katika mahusiano ambayo hayakuwa na uelekeo, niliumia
sana mpaka pale nilipogundua kuwa sikupaswa kuishi kwaajili ya mtu. Kama
ipo ipo tu, niliamua kufanya maisha yangu mwenyewe kujiimarisha mimi
kwanza kama mwanamke ndipo niwaze wengine.
Nilikuwa na mwanaume ambaye baada ya
mahusiano ya miaka mitatu, wote tukiwa tunafanya kazi alikuwa bado
hajamaliza ujana na alitaka tuendelee kutoka kila mwisho wa wiki kunywa
na kufurahi na rafiki zake, nilikuwa na mwanaume ambaye ukimuuliza
mipango yake ya maisha ya baadaye anakuambia “Mbona unaharakisha mambo…”
akidhani labda namuulizia unanioa lini?
Nilikuwa na mwanaume ambaye
ukimuambia kiwanja kinauzwa sehemu flani anakuambia sina pesa lakini
mwisho wawiki anakuambia twende Zanzibar tukapumzike. Ingawa najua kwa
baadhi ya mabinti wengi anaweza kuwa mwanaume wa ndoto zao, lakini mimi
wakati huo sikuwa binti tena, miaka 27 tayari nilishakuwa mwanamke na
nilipaswa kuwaza kuhusu maisha ya mbeleni kuliko burudani.
Niliamua kuachana naye kwakuwa
nilikuwa sioni uelekeo, tayari alishaanza kunipoteza, ingawa
sikubadilisha mawazo kwa maana bado niliendelea kubaki na malengo yangu
ya kimaisha, lakini mambo yake yalinirudisha nyuma. Nilijikuta naingia
katika matumizi ya kipuuzi kwajaili ya kulinda penzi, mpo club kaishiwa
kama mwanamke inabidi nitoe hela yangu kuokoa jahazi. Baada ya kuona
napotea basi niliamua kujitoa na kuanza maisha yangu bila yeye.
Leo hii nina kampuni yangu, ndoa
yangu na familia niliyokuwa nikiitamani, sikusubiri mwanaume kutimiza
ndoto zangu nilianza kuziendelea ndoto zangu mimi mwenyewe. Hata wewe
unaweza kama utatambua thamani yako, kama utafahamu kuwa hakuna mwanaume
yeyote ambaye anaweza kukuinua kama wewe mwenyewe hutaaamua kuinuka.
Kama huoni dalili za mtu uliyenaye
kubadilika, kukua, kuwa mtu mzima ni vyema ukajitoa na kufanya mambo
yako ya kiutu uzima. Mtu sahihi atakuja na atakupa furaha ya kweli. Acha
kujilazimishia kuwa labda unapenda sana, kama umefika wakati unaona
kabisa mtu uliyenaye sio kwamba tu hataki kubadilika lakini pia
anakubadilisha taratibu na unaelekea kuwa kama yeye, basi ni wakati
sahihi wa kuachana naye.
No comments:
Post a Comment