Kuna baadhi ya wanaume ambao wanajiskia kuwa na furaha wakiwa na
marafiki zao wa kike ambao wanawapenda kisiri, lakini kama umechoshwa na
kuboeka kuwa rafiki pekee na mwanamke unayempenda, basi huu ndio wakati
mzuri wa kujeuza gemu yako kabisa. Barabara ya
kumbadilisha rafiki yako hadi kuwa girlfriend wako inaweza kuwa ndefu,
lakini mwishowe huwa na utamu wake. Halafu kama wewe ni mwoga, mpweke,
ama bikra ambaye hajui lolote kuhusu jinsi ya kuwatongoza wanawake, basi
usitie shaka. Huwa ni rahisi kutimiza hili. Na utaweza kujenga
confidence yako na kujeuka mwanaume ambaye anaweza kujumuika na
kutangamana na wengine kirahisi. Hii hapa ni njia nzuri zaidi za
kukuwezesha kumvutia mwanamke wa ndoto yako na finally ajeuke zaidi ya
rafiki yako. Hivi ndivyo unavyopaswa kufanya.
#1 Acha tabia ya kuwa Mr. Mzuri
Ijapokuwa ni vizuri kuwa mwanaume mzuri mara moja au nyingine, kuwa
mzuri sana kiasi cha kuwa unaonekana kama unajipendekeza kwa mwanamke
hakufai. Mwanzo ukiendelea kumuonyesha uzuri wako kila wakati utabakia
kuwa rafiki yake milele. Kama hujawahi kugundua hili, wanawake wengi
huwa wanapendezwa zaidi na wanaume ambao ni masharobaro ama ‘bad boys’.
Hii ni kwa sababu masharobaro huwa wanaonyesha hulka ya kutojali ama
kuwa na hulka ambazo huonyesha ubaya wao mara moja au nyingine – hii
huwavutia wanawake sana. Wanawake hupenda wanaume ambao wanaonyesha
confidence – kitu ambacho mwanaume alpha huwa anamiliki. Well, wanaume
ambao wanatawala na ambao wanaonyesha kucontrol katika kila hali huwa
kikawaida wanakuwa na confidence wakati wote. So, kama utaanza kuiga na
kuonekana kama mwanaume sharobaro, unaweza kujeuka na kuonekana na mvuto
na nishati zaidi ambayo itakuweka juu katika mashindano kwa muda mfupi
sana.
#2 Usimuandame kama kelbu
Kama unapenda kumfuata fuata mwanamke kama kelbu, basi ataudhika na wewe
na mwishowe atakuacha katikati. Mbaya zaidi anaweza kuambia marafiki
zake kuwa wewe ni fala usiyekuwa na kazi ya kufanya. Ama anaweza
kukatiza urafiki wenu. So, njia nzuri ya kufanya kwa sasa ni kurelax na
utulize gemu. Kwa njia nyingine ni kuwa, usimkimbize kufanya jambo
lolote. Ukitaka kumfanya mwanamke awe interested na wewe kiharaka ni
kwa kuhakikisha ya kuwa unakuwa mtu asiyeeleweka, yaani leo uko na yeye,
kesho uko busy hupatikani. Huku kutamfanya akumisi na kutaka kuspend
muda wake mwingi na wewe.
#3 Usikubaliane na kila kitu
Kama utaendelea kufanya kila kitu ambacho mwanamke anakuambia ama
kukubaliana na kila kitu anachotaka, basi ataanza kukuchukulia advantage
kwa sababu atagundua kuwa amekuweka katika viganja vyake. Jithamini
wewe mwenyewe zaidi kuanzia sasa na umuonyeshe kuwa haubabaikii ama
kuomba atenshen kutoka kwake. Hii itamfanya kuanza kujishuku na
itamfanya kutaka kujua kwa nini umekuwa tofauti. Baadaye, ataanza
kukukimbilia ili abadilike.
#4 Isome na uielewe sanaa ya kutongoza
Katika dunia ya kudeti na kutongoza, hakuna kitu kinachofanya kazi
vizuri zaidi kama kushawishi. Mwanzo, hakuna kitu ambacho kitatokea kati
yako na rafiki yako kama hujui kushawishi. So, nenda ujifunze jinsi ya
kutumia macho yako kumtongoza rafiki yako, mpe tabasamu, mfinyie jicho,
na mhusishe katika gumzo ambalo litampa hamu ya kukukaribia. Fanya haya
yote na utaona utofauti wa rafiki yako akianza kufall na wewe pole pole.
Utajipata rafiki yako amejeuka kuwa mpenzi wako.
No comments:
Post a Comment