1. KUHONGA HUBORESHA MAPENZI:Fahamu kuwa unapomhonga mpenzi wako
unamfanya ajihisi kama ni wapekee kwako, atajiona kama ni mmoja wapo
kati ya watu wenye thamani kwako na huamini kama kweli upo karibu yake
na unamjali.
Hali hii humfanya yeye kushindwa kutolipa mazuri kwako.
Wengi kabla ya kuomba papuchi hutanguliza hongo kwanza, si lazima iwe pesa hata hongo ya sifa za uongo na ukweli.
Kwa kuhonga kwako inamlazimu na yeye kulipa fadhila kwa kuonesha upendo wa dhati na utamfanya azidishe mapenzi kwako.
2. KUHONGA KUNAJENGA SANA KUMBUKUMBU KATIKA MAPENZI:
Fahamu kuwa unapomhonga mpenzi wako inakusaidia wewe kujijenga katika
mawazo yake na endapo kama itatokea mkaachana nae basi pindi mpenzi wako
atakapokuwa anaziona zawadi zako zitamfanya akukumbuke kwa mengi na
atahisi kama kuachana na wewe kwake kuna tofauti na atajihisi kupoteza
vingi toka kwako na kamwe kumbukumbu yako kwake haitofutika kila
anapoona vitu ulivyomhonga.
Jitahidi sana unapohonga usihonge pesa tu, honga vitu vya kudumu maana
huwa asset yako ya baadaye, pindi unapotokea mkwaruzano baina yenu.
Pesa huwa ni hongo inayovutia kwa muda mfupi na husaidia kupata kile
unachokitaka kwa muda mfupi, ila jua atazitumia zitaisha utakuwa
hujajenga misingi imara ya mapenzi.
Simaanishi kuwa usimpe mpenzi wako hela, hapana ila inabidi ufahamu kuwa
pesa hutumika katika kukidhi mahitaji na sio katika kuboresha mapenzi.
Aisee jifunzeni kuhonga mpunguze stress za mapenzi
No comments:
Post a Comment