Ni miezi miwili sasa tangu nimeacha kazi kampuni ya zamani, na sasa nipo
kwenye kampuni nyingine, hii kazi mpya nimetafutiwa na Boss wangu ambae
ndie mkuu wa idara yetu, nimepanda cheo kidogo, kule nilikuwa Karani na
huku kupya mimi ni Supervisor.
Sasa huyu Boss alieniingiza kazini nimekua na urafiki nae tangu
nimeingia hapa, kitu kinachonikwaza ni mwenendo wa huyu Boss wangu,
yaani nimekua kama mtumwa, wakati wote anataka tufanye ngono, jioni
wakati wa kuondoka anataka tubaki ofisini kwake, najikuta nafika home
saa tatu hivyo kumkuta Mr wangu amesharudi Muda, inakua ugomvi, inabidi
nimdanganye kuwa kazi mpya imekua too demanding kwangu, nachelewa
kutoka.
Weekend ni hivyo hivyo, inabidi nisingizie home kuwa tunatakiwa kazini
hata Jumapili, nimejikuta naishi kama mtumwa kwa sababu ya hii kazi
aliyonipa huyu Boss, maneno maneno yamekua mengi hapa kazini miongoni
mwa Staff wenzangu kuhusu mwenendo wangu na huyu Boss, nina wasi wasi
maneno haya yanaweza kumfikia Mr wangu ikawa shida.
Natamani kuirudia ile kazi yangu ya awali, kazi hii mpya napata mshahara
mzuri lakini nimekua kama mtumwa, wakati mwingine nikionesha dalili za
kumgomea kubaki jioni anakua mkali na kuanza vitisho kwamba eti ''
unasahau nani kakuweka hapo ''Inabidi tu nishiriki nae ingawa sipendi.
No comments:
Post a Comment