MSAIDIENI HUYU MSICHANA:
Pole na kazi Mpekuzi, Mimi ni msichana mwenye umri wa miaka 22, nina
rafiki yangu ambaye nimesoma naye na ni kama ndugu yangu wa damu
kutokana na tulivyo na watu wote wanajua kwamba mimi ni yeye na yeye ni
mimi.
Rafiki yangu huyu nimesoma naye kuanzia O-leve, mpaka advance na sasa
tupo wote chuo hapa dar es salaam, kwa kifupu ni urafiki wa damu.
Mwaka jana katikati rafiki yangu huyu alinitambulisha kwa boyfriend wake
ambaye ni kaka anayesoma chuo kingine ambacho hakiko mbali na chuo
chetu, kwa kweli wanapendana sana na ni kaka mzuri sana ambaye rafiki
yangu anajivunia kuwa naye, na kutokana na ukaribu wangu na rafiki
yangu, nimekuwa nikiwasiliana sana na shemeji yangu huyu kiasi kwamba
naye amekuwa ni mtu wa karibu sana, na muda wowote asipompata rafiki
yangu amekuwa akinipigia mimi, na hata mara nyingine tumekuwa tukienda
matembezeni watu watatu, yaani mimi rafiki yangu na shemeji, ukaribu
nilionao na shemeji yangu huyu umenifanya nianze kumthamini na kumjali
hadi naogopa, mara ya kwanza nilidhani ni kwa sababu nampenda rafiki
yangu, lakini kwa sasa naona imepitiliza na nimegundua kwamba nampenda
huyu kaka na natamani siku nifanye naye mapenzi sababu mimi nipo single
kwa sasa kwakuwa nilikorofishana na aliyekuwa mpenzi wangu.
Hali imekuwa mbaya kwani hata sasa naona hata huyu shemeji yangu nae
ananipenda lakini hawezi kuniambia, natamani siku aje hostel wakati huyu
rafiki yangu hayupo ili alale hapa hapa.
Kwa kweli nimechanganyikiwa kwa kifupi nahisi kuumwa kwa sababu nina
mpenda kupita maelezo sema nahofia kumuumiza rafiki yangu kwani najua
siku nikimpindua lazima shemeji amuache rafiki yangu aje kwangu sababu
nina shepu ya kumtamanisha mwanaume yoyote.
Naombeni msaada wana jamii.
No comments:
Post a Comment