Nilishawahi kusema huko nyuma kwamba,
mapenzi yanachukuwa sehemu kubwa sana ya maisha yetu ya kila siku.
Tunafanya kazi usiku na mchana lakini pesa tunazopata tunazitumia kwenye kufurahia maisha na wapenzi wetu.
Ndiyo maana ukiwa huna mpenzi wakati
unahitaji kuwa naye au unaye lakini anakukorofisha, hata mambo mengine
huwezi kuyafanya kwa ufasaha. Lakini yule ambaye maisha yake ya
kimapenzi yako sawa, anapata anachokitaka kutoka kwa mpenzi wake,
utagundua anafanya kazi kwa ufanisi mkubwa na furaha haikauki. Wakati
ukweli ukiwa hivyo, wapo ambao wanaachika kila siku kwa sababu ya
kushindwa kujua namna ya kuwashika wapenzi wao.
Kuna ambao kusalitiwa kumekuwa ni sehemu
ya maisha yao kwa sababu hawajui yapi wayafanye ili wapenzi wao
wasifikirie kutoka nje ya uhusiano wao. Kimsingi nimegundua wengi hatuna
elimu ya kutosha juu ya mapenzi. Unakuta mtu kaanzisha uhusiano na mtu
ambaye yuko mbali lakini hajui wanawezaje kulidumisha penzi lao.
Mmeoana wote mnafanya kazi na ni
wanandoa, mnawezaje kuishi katika msingi sahihi? Hayo yote utayajua
endapo tu utajua sehemu sahihi ya kuweza kujifunza na kuwa na ufahamu
kuhusu mambo hayo.
Huenda wewe tangu umezaliwa hujawahi
kujihusisha kimapenzi, leo umeingia kwenye uhusiano na hujui chochote,
kama huna elimu ya mapenzi hata kama umzuri vipi, utaachika tu kama siyo
kusalitiwa kila siku.
Ndiyo maana leo nimeleta mada hii ili
kama ulikuwa hujui, uanze leo kujiimarisha kwenye masuala ya mahaba.
Kumbuka hapa nazungumzia mapenzi ya kiutu uzima, yale ambayo huwezi
kufundishwa shuleni.
1. Mtandaoni
Mitandao imekuwa ni msaada sana katika
ulimwengu wa sasa. Hakuna ambalo utalihitaji usilipate kwenye mtandao.
Kwa maana hiyo basi, kama kuna jambo unataka kulijua kuhusu mapenzi,
kuwa rafiki wa mitandao husika.
Kwa mfano unataka kujua jinsi unavyoweza
kumfurahisha mpenzi wako mkiwa faragha. Ukiuliza mtandao,
utakuletea.Licha ya kwamba lugha unayotumika ni ya Kiingereza, naamini
wengi wetu tunajua hata kama ni cha kubangaiza. Ila zipo baadhi ya mada
ukiandika kwa Kiswahili pia unaweza kuzipata.
2. Majarida maalum
Yapo majarida yanayozungumzia mapenzi
kwa undani wake ambayo yanauzwa sehemu maalum kwa jili ya watu wazima
tu. Kama kweli wewe ni mtu mwenye uhitaji wa majarida hayo, ukiulizia
utayapata kwani huwezi kuyakuta yanauzwa kiholela.
Wakati mwingine yanauzwa bei kubwa
lakini elimu utakayoipata ni kubwa na huwezi hata kujutia fedha
uliyotoa. Kwa mfano unanunua jarida la shilingi 50,000 na ndani yake
ukapata mada juu ya kuishi kwa furaha na mpenzi wako, namna na
kuidumisha ndoa yako, jinsi ya kumpagawisha mpenzi wako muwapo faragha
na kadhalika. Huoni itakuwa ni pesa ndogo ukilinganisha na gharama
ulizotumia kwenye harusi yenu?
3. Ongea na wataalam
Kuna wataalam wa mambo ya mapenzi ambao
wanaweza kukusaidia. Kwa mfano mimi nimekuwa nikitumia muda wangu mwingi
kushauri wasomaji wangu juu ya mambo yanayowakosesha furaha katika
maisha yao ya kimapenzi.
Siyo mimi tu, wapo wengi wakiwemo baadhi
ya akina mama ambao wamekuwa wakitumika sana kwenye kuwafunda wasichana
kabla ya kuingia kwenye ndoa.Kikubwa ni kujua watu sahihi wa kuwauliza
mambo sahihi kuhusiana na mapenzi. Nilichogundua mimi ni baadhi ya watu
kuwa na aibu. Hivi unaonaje aibu huku unataka kujua mambo nyeti ambayo
unajua kutokuyafahamu kunaweza kuihatarisha ndoa yako?
4. Angalia vipindi vya kikubwa
Kwa watu wenye uchu na elimu hasa hii
nyeti, inabidi wakati mwingine wakubali kuamka usiku na kuangalia
vipindi ambavyo vinazungumzia mapenzi kwa watu wazima.Mara nyingi
vipindi hivi huwezi kuviona mchana, wanaovirusha husubiri muda ambao
watoto wamelala. Ukiwa ni mpenzi wa kuvifuatilia vipindi hivi, ni lazima
utakuwa bora kwenye uhusiano wako.
5. Nunua CD
Huenda hata wewe una CD zako ambazo mara
nyingi unaziangalia usiku kabisa, ukiwa peke yako au na mwenza wako.
Hilo ni jambo zuri hasa linapokuja suala la kujiweka fiti kimapenzi.
Katika hili naomba niseme tu kwamba,
kuna ambao wanazitumia CD hizi kujiharibu. Wanazinunua ili kujifunza
mambo kadhaa lakini mwisho wake wananogewa na kujikuta wakimaliza haja
zao kwa kuziangalia.
Niwaonye tu kwamba, ukizoea sana
kuziangalia picha hizo ukiwa peke yako kisha ukamaliza shida zako,
unaweza kujikuta si mtu unayependa kuwa na mpenzi tena. Wapo ambao leo
hii hawataki kusikia kitu mpenzi, kisa wakiangalia CD hizo humaliza haja
zao! Ni sawa unaweza kumaliza haja zako lakini madhara yake ni makubwa.
Ndiyo maana nasema kwamba, tumia CD hizo kujipatia ujuzi lakini si
kumalizia haja zako.
Ni hayo tu ila kama unataka kujifunza
zaidi kupitia mimi, usisite kunitafuta. Kumbuka ujanja na ubunifu wako
ndivyo vinaweza kudumisha ndoa yako lakini ukiwa unaendesha maisha yako
kibubusa, kaa mkao wa kusalitiwa kama siyo kuachwa!
No comments:
Post a Comment