Artikel Terbaru

Responsive Ads Here

Saturday, March 24, 2018

Nina wasiwasi huyu mtoto sio wa kwangu maana mimba imedumu kwa muda mfupi tangu anipe taarifa


Niende moja kwa moja kwenye habari apo juu,nakumbuka mwezi wa saba 2017 nilipata nafasi ya kwenda CHUO CHA VETA Babati ,Manyara. Hapo chuoni niliazisha mahusiano na mwanamke ambaye tulikuwa tunasoma wote VETA .

Mara ya kwanza kwenye mahusiano demu alinizingua nikamuacha,niliendelea kumfutilia mwezi wa Tisa 2017 demu alinikubalia, mahusiano yetu yakawa mazuri.

Tarehe 22/09/2017 ilikuwa mara ya kwanza Kusex naye,zilipita wiki mbili mbele demu akasema ana MIMBA ,tulipima kweli mimba ikawa imo kweli. Nilimpenda na yeye alinipenda, mwezi wa pili 2018 alienda nyumbani kwao akawa anipigia simu anaumwa; baada ya muda si mrefu alinipigia baba yake akasema "kwa nini hutaki kuja nyumbani" nikamwambia baba nitakuja.

Tarehe 18/03/2018 Alinipigia simu akasema amejifungua mtoto wa kiume.
Nilishangaa sana inakuaje mimba ya miezi sita ujifungue nilimwambia ;akasema usikatae hii mimba ni yako kabsa mume wangu.

Nilimwambia hiyo mimba sio yangu mtafute mwanaume aliyekupa mimba hiyo.

Naombeni ushauri wenu.
Hakuna mimba ya miezi sita na amekili kabisa mtoto miezi imekamilika tisa na hana tatizo mtoto.

No comments:

Post a Comment