Baba yangu mzazi kaja juzi kutoka kijijini kwa matibabu.Nilimkatia
tiketi ya ndege akapandie mkoani, mke wangu akadai ni uharibifu wa pesa
kumsafirisha Mzee kwa ndege angepanda basi wakati mzee wake mwezi
uliopita alikua hapa kwetu na kaja kwa ndege kwa hela yangu wakati
haumwi ni mzima na baba yangu alikua mgonjwa.
Kana kwamba hiyo haitoshi mizunguko yote ya muhimbili naenda mm na ndugu
zangu Wa ukoo yeye yupo busy na kazi, anaenda kwa kusukumwa mno.
Ukiachana na hilo hata misiba ya ukoo wetu either atatafuta sababu
inayokaribiana na ukweli asiende au ataenda akifika pale anageuka mgeni
hashughuliki na chochote.
Wazazi wake wakiwepo hapa itakua ni kama wageni wametoka ulaya
nitapigiwa simu nije na grant, sijui ninunue jack Daniels kwamba baba
anapenda sana hiyo pombe njoo nayo dear.Weekend tuwapeleke wazazi wake
beach yaani inakua ni mikiki ndani.
Tofauti na wazazi wangu wakija hakuna kinachoendelea ndani, hakuna
mabadiliko ya vyakula wala nini mimi kwa kuepusha shari huwa namwambia
baba twende tukale bar maana anatakiwa ale vyakula chukuchuku au vya
kuchoma.
Jana usiku baba aliniuliza kuwa huyu mwanamke mlifahamiana muda gani
kabla ya kuoana nikamwambia miaka 4 akasema si kweli
hakuamini.Nikajiuliza kwa nn baba kaniuliza swali hili.
Hayo yote ni Tisa Kumi hufanya mambo yake ya maendeleo kimya na kwa siri
kubwa humtumia mdogo wake wa kiume kufanya hayo yote I.e kujenga kwa
siri. Nikiamua kumweka chini kwa utulivu na kumuhoji kikao hubadilika na
kuwa vurugu tupu kwamba namfatilia, kwamba simpi nafasi apumue, kwamba
mwanaume nina gubu mimi.
Anyway mimi ni mfanyakazi wa shirika la kimataifa, nina masters, wife ana bachelor degree yeye ni banker
Tuna watoto wawili mmoja yupo primary school standard one na mwingine nursery school.
Wakuu nawauliza hivi:-
(1) Hili ni hali ya kawaida kwa ndoa zote?
(2) Inawezekana sikumfaham huyu mwanake kwa undani?
(Relationship 4 years) je muda huo hautoshi kumjua mtu? Au alificha?
(3) Nimuite mzee yupi kuja kuzungumza nae maana wazee wote wa ukoo wangu anawaona hawana maana
(4) Kuna yeyote kati yenu ndugu zangu wana JF mwenye shida kama hili? Na aliitatuaje?
(5) Wazazi wangu wamechoka na hali hii niwaeleze nini wanielewe?
(6) Nimfanyeje mwanamke huyu?
Naomba ushauri wenu kwa dhati ya moyo wangu maana mimi mwenyewe nimechoka na hali hili iliyodumu kwa miaka 8
Sasa nafikiria REGIME CHANGE
NB: Sijawahi kuchepuka ila kwa sasa ndo nimeanza kufikiria replacement
Sunday, June 10, 2018
Hivi Wanandoa Wenzangu na Wake Zenu pia Wako Kama Huyu Wangu?
About Anonymous
Soratemplates is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of templatesyard is to provide the best quality blogger templates.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment