Utafiti uliochapishwa katika Jaida la British Journal of Psychology,
ulibaini kuwa wanaume huwachukulia wanawake ambao ni warembo kama vyombo
vya starehe tu.
Utafiti umeonyesha kuwa wanaume wengi wanapendelea kuwa katika mahusiano
ya muda mrefu na wanawake wasiokuwa na mvuto sana ikilinganishwa na
wanawake wenye mvuto (warembo).
Baadhi ya sababu kwa nini wanaume wanapendelea kuwa katika mahusiano na
wanawake wenye mvuto na warembo badala ya kuwaoa ni pamoja na;
Utafiti uliofanyika hapo awali ulibaini kuwa wanawake wenye mvuto ni
rahisi zaidi kutokuwa waaminifu ndani ya mahusiano hasa pale wapenzi wao
wanapokuwa hawana mvuto. Wanaume wengi huwa na wasiwasi pale wanapokuwa
mbali na wapenzi wao, huwa wanakuwa na maswali mengi
Wanawake wenye mvuto hutafuta umaarufu. Wanaume hupenda wanawake
wasiokuwa na mambo mengi, lakini kwa upande wa wanawake warembo
inaonekana kuwa wao hujali zaidi muonekano wao na mvuto wao wa nje
kuliko walivyo ndani (tabia na mwenendo) hivyo kukosa sifa za kuwa wake
bora. Ni vigumu sana kuendana na baadhi ya matakwa ya wanawake warembo.
Sababu nyingine ni kuwa, wanawake wenye mvuto na warembo hutajwa kuwa
ghali (inahitaji gharama kubwa kummudu mwanamke wa aina hii).
Hili linaangalia zaidi aina yao ya maisha. Wanawake hawa hupendelea
kuvaa nguo za gharama, kuishi maisha ya starehe na kufanya vitu ambavyo
vinahitaji gharama kubwa, hivyo wao hupendelea kuwa na wanaume ambao
wana kipato cha kutosha kuwahudumia mahitaji yao yote.
Monday, June 11, 2018
Unajua Kwanini Wanawake Warembo Hawaolewi?
About Anonymous
Soratemplates is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of templatesyard is to provide the best quality blogger templates.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment