Aliyekua rais wa Uruguay, Jose Mujica ambaye alifahamika kama rais
maskini zaidi duniani amesema hatachukua malipo yake ya uzeeni tangu
aanze kuhudumu kama seneta.
Mujica aliacha kazi ya useneta siku ya Jumanne kiti ambacho amekua
akishikilia tangu muda wake wa kuhudumu kama raisi ulipo kamilika mwaka
2015.
Kwa mujibu wa BBC rais huyo mstaafu alidai kuwa amechoka na hangeweza
kuendelea na kazi hadi mwaka wa 2020. Muasi huyo wa zamani wa mlengo wa
kushoto ana miaka 83.
Mujica aliwasilisha barua ya kuacha kazi kwa mkuu wa seneti. Alisema
kwamba fikra ya kuacha kazi ni ya kibinasfi huku akiongeza kuwa ni
uchovu wa safari ndefu.
Hata hivyo aliongeza kua ataendelea kuchangia hoja kwa sababu bado akili
yake inafanya kazi. Mujica anayejulikana kwa matamshi yake ya kichesi
aliomba msamaha kwa wenzake kwa uamuzi huo.
Mwaka 2016, alidai rais wa Venezuela Nicolás Maduro ni mwendazimu kama
mbuzi. Umaarufu wake ulienea kutokana na maisha yake ya chini ya kukataa
kuishi kwenye Ikulu ya rais.
Wakati akiwa rais na hata sasa yeye pamoja na mkewe ambaye pia
alimsaidia katika vita vya msituni wamekua wakiishi katika shamba moja
nje kidogo mwa mji wa Montevideo.
Alitoa mshahari wake kwa misaada na kile alichobaki nacho tu alipoingia
ofisini mwaka wa 2010 ni gari aina ya Volkswagen Beetle la mwaka 1987.
Gari hilo lilipata umaarufu na mwaka 2014 alipewa dola milioni moja
lakini akakataa huku akidai kuwa atashindwa kumbeba mbwa wake mwenye
miguu mitatu.
Kuacha kazi kwa Mujica hakukupokelewa na mshangao kwa sababu alikua
amedokeza kufanya hivyo mnano Agosti 3 alipofika mara ya mwisho seneti.
Wakati huo, mahasimu wake wa kisiasa walisema hawakua na uhakika ya
kwamba atastaafu. Seneta Luis Alberto Heber alidai kuwa Mujica aliacha
kazi ili ajipange kuwania kiti cha urais mwaka 2019 kwa mara ya pili.
Huku wenazke katika seneti wakimjalia mazuri wakosoaji waliendeleza
mijdala kwenye mitandao ya kijamii wakidai aombe msamaha vitendo
alivyofanya wakati akiwa mwanachama wa waasi wa Tupamaros miaka ya 1960
na 70.
Monday, August 20, 2018
Rais Maskini zaidi Duniani Akataa Malipo yake ya Uzeeni
About Anonymous
Soratemplates is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of templatesyard is to provide the best quality blogger templates.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment