Artikel Terbaru

Responsive Ads Here

Monday, April 30, 2018

Jinsi Ya Kumbemba Mwanamke Kwa Kutumia *Sanaa Ya Kiza* + Viini Macho

Utafiti tuliokuwa tukiufanya kwa blog hii ya Nesi Mapenzi tumegundua ya kuwa kuna asilimia kubwa ya watembeleaji wetu ambao wangependa machapisho ya sanaa ya kuwashawishi wanawake kutoka kwa waume zao. Katika msururu wetu wa kuanza kutumia sanaa ya kiza, tutakuwa kukieleza na kutumia mbinu ya saikolojia siri, miendelezo shaushi, mazungumzo viini macho katika kumfisidi mwanamke.

ONYO: kuna baadhi ya watu ambao wanaweza kuona machapisho aina hii kukosa maadili kijamii. Kama utaona kuwa utazilika ama kuudhika na post hizi, tafadhali itakuwa vyema kama hautaendelea kusoma zaidi ya hapa.

So katika msururu wetu wa machaposho aina hii tumeanza na:


Jinsi ya kumshawishi mwanamke kutoka kwa mwanaume mwingine

Katika post ya mbeleni tulieleze kwa upana jinsi ya kumtongoza na kumshawishi mwanamke ambaye ana boyfriend, leo tumeamua kuingia kwa undani zaidi kwa kutumia sanaa ya mazungumzo kwa kutumia mbinu ya kiini macho kumfanya amchukie boyfriend wake.
Kabla kutumia mbinu hii, lazima mwanaume ajenge uhusiano mwema baina yake na mwanamke. Kuwa na uhusiano mwema baina yako na mwanamke kutakupa wewe uwezo wa urahisi kufanya kile ambacho unataka kwa mwanamke yeyote.
Ok. Tukirudi kwa sanaa hii, kile ambacho unafaa kufanya ni kutumia maswali ambayo yamepakizwa tayari na ambayo yatamfanya yeye kujipima thamani yake.... halafu utamlazimisha kugundua ila zote za mpenzi wake/boyfriend. Ni fioa, siri, na mbinu ya kuzimu.
Hili ndilo swali la ulozi ambalo unafaa kuanza kumuuliza:
'Unajua nini, nimekuwa na shauku kutaka kujua ni sababu gani mwanamke anashikika sana kwa mpenzi wake. Ni kitu gani cha kwanza ambacho kilikuvutia kwa boyfriend wako?'
Mara ya kwanza ataliona swali hili ni geni kwa nini umetaka kujua zaidi kumhusu boyfriend wake, lakini kile ambacho unataka ni kumfanya yeye kuelezea kumhusu boyfriend wake zaidi kadri iwezekanavyo. So unafaa kuufuata mkondo huu wa maswali-
- "ni kitu gani unachopenda kumhusu?"
- "kiukweli unamhisi vipi hisia zake kwako? (muulize zaidi)
- "katika fikra zako kidunia, ungetamani kuwa na boyfriend kamili mwenye sifa zipi?" (mfanye ayafananishe matamanio yake)
Kile ambacho unafanya hapa ni kumpa nafasi ya kipekee ya kuongea mabaya kumhusu boyfriend wake. Wakati ambapo ataanza kuingia kueleza mambo hasi kumhusu boyfriend wake, mhimize aongee zaidi kwa kumuuliza aeleze kwa kina. Mfano akisema "nachukia tabia ya boyfriend wangu kunikasirikia kwa sababu ndogo ndogo" wewe unaweza kumuuliza "kukasirika kwa sababu kama zipi zinazokuudhi?" nk.
Ok. Hii hapa ni mbinu ya maswali ya kumuuliza kumfanya aue hisia zake za boyfriend wake asilani -tumia saikolojia mjeuko kumfanya akudhihirishie kuwa boyfriend wake ni mbaya.
-"bila shaka hakugundua kama alikuwa akifanya..."
-"lakini anaonekana si mbaya sana..."
-"labda amekuwa akifanya hivyo kwa sababu wa mapenzi yenu..."
Ujanja hapa ni kuwa MSIRI iwezekanavyo, na haufai kumfanya agundue ya kuwa unafanya amfikirie boyfriend wake kama mtu mbaya.  Iwapo wewe una azma ya kuwa mwangamizaji wa mahusiano basi unafaa kufahamu jinsi ya kutumia mbinu hii ili kumfanya mwanamke akupende bila yeye kuelewa sababu za kwake kukuzimia. 
Kama wataka kujua mbinu hii kwa kina fanya kulike page ya Nesi Mapenzi na mtoe request nyingi kupitia kwa inbox ili admin wa blog hii aweze kuidhinisha post inayofafanua zaidi.

Makosa 5 Ya SMS Ambayo Unamfanya Mwanamke Akucheke Na Kukuona Jinsi Ulivyo Mjinga

Kila mtu hutumia SMS kila siku kuwasiliana.

Kama inavyotambulika ni kuwa ni rahisi sana kutumia jumbe fupi kuwasiliana na mwingine kupitisha ujumbe. Lakini je huo ujumbe unaoutuma unachukuliwa vipi na unayemtumia?
Katika swala la kutongoza ama kumSMS mwanamke, wanaume wengine wanafanya makosa makubwa wakati wanapochat bila wao kujua. Jambo ambalo nimeamua kuliweka wazi. 
(Kwa bahati mbaya ni kuwa makosa haya yanafanywa na wanaume kila wakati)
1. SMS za kujisifu
Kosa hili nishawahi kulizungumzia mara kwa mara kwa blog hii, na ni wanaume wengi sana wanapenda kulifanya. Najua waelewa nazungumza kuhusu nini. Kuongea stori za kirare (na 85% ya ufala) ambazo unajaribu kumwonyesha mwanamke jinsi ulivyo burudi, kumwonyesha kuwa una marafiki wazuri ambao wanaweza kukufanyia chochote kile utakacho, na kuwa huwa unatembea sehemu tofauti tofauti za kifahari kwa kuwa umefanikiwa na una umuhimu mkubwa katika jamii.
Kwa maneno ya urahisi ni kuwa unajaribu kadri iwezekanavyo kumpendeza mwanamke.
Mwanamke wako mwenye hadhi atayaringa macho yake na kucheka kimoyo akianza kuhisi kama unafanya hivyo kumpendeza. Kwa nini? Kwa sababu unajaribu kutumia mbinu hio kumfanya akupende. Ni wakati wako wa kuacha kutumia mwanamke meseji kama hizi.
2. Kuwa na mapepe
Kumualika mtoke deti pamoja kabla ya kutumia mbinu ya kumtongoza ili akukubali. Hakuna njia nyingine nzuri zaidi ya hii kudhihirisha kuwa wewe:
(a) una experience ndogo ya kutangamana na kuwajua wanawake (b) hauna ladha ya maana kuchagua wanawake
(PssS: Kama kujuana kwenu kulikuwa kwa nishati, unaweza kuipuuza hii)
3. Kupumbazika kwake
Unamtumia mamia ya text za ucheshi, unamsuka, unamwelezea stori za ovyo ovyo za abunuwasi na nyingine, na unazidi kumtumia sms za 'kumvutia' zaidi --mpaka inafikia mahali flani unamboa na anaanza kukupuuza.
So imekuwaje mpaka ameanza kukupuuza? Umempandisha mzuka wa kukupenda halafu ukapoesha kila kitu.
Wanawake wanadhania ya kuwa mwanaume ambaye anaonyesha interest kwao halafu hataki watoke deti pamoja huwa ni mwoga wa kuchukua hatua ya mbele.
4. Kuharibu tenshen
Unafafanua jokes zako kuhakikishia ya kuwa anaelewa kile unachomaanisha. Unajihisi haujiskii vizuri kama hujibu texts zake, kwa sababu hutaki aone kama unampuuza. Kama anakataa na kitu flani, unanyenyekea na kukubaliana na kila atakachosema.
Hii inaonyesha ya kuwa wewe si mwanaume dhabiti, kwa sababu hauwezi kuhimili tenshen, na mbaya zaidi ni kuwa unaogopa kumpoteza.
5. Mambo yakienda mrama
Wakati ambapo amekataa ama kusimama kureply text zako, unaanza kutoa kucha zako za ujinga na ''kumweka sehemu anayostahili''
Unaanza kumwambia jinsi alivyo mbovu, anatisha, ni zuzu ama mpotezea watu wakati, ama ni mwanamke mwenye hadhi ya chini na unaweza kufanya zaidi. (Kwa mwanamke atakuwa akifikiria, ''Ha ha, haukuwa unasema hivyo dakika mbili zilizopita ulipodhania una nafasi kwangu'')
Okay...
Najua kuwa text zako ni za level ya juu wakati unapomtext mwanamke, na naamini hauwezi kufanya makosa tuliyoyaeleza hapo juu. Lakini tukiwa waadilifu ni kuwa tunaweza kukubali kufanya kosa moja au lingine katika haya.

Tambua Kama Mwanamke Anakupenda Kwa Kuangalia Miguu Yake

Hebu fikiria situation ambayo unaongea na mwanamke mrembo. Unamskiliza kila kitu anachozungumza... Unamwangalia jinsi vile midomo yake inavyojishepu wakati anapoongea maneno flani, na kumakinika na umbile lake kila wakati anapotaja maneno fulani na pozi tamu.

Fikiria sahizi unatatizwa kumakinika na vile anavyounembua mwili wake... vile anavyokaa... na jinsi anavyokunywa kinywaji chake mbele yako...

Lakini haya yote yakiendelea, unaongea na yeye bila kusitasita wala kubabaika, bila kuonyesha ishara yeyote ya kuwa umbo lake linakuchanganya akili. [Soma: Jinsi ya kuzungumza na mwanamke]

Utakuwa unadhania ya kuwa unaelewa kila kitu ambacho anatamka kutoka kwa mdomo wake. Kama unaamini hivyo, basi fahamu ya kuwa unajidanganya.

Wanaume wengi hudhania ya kuwa wanaweza kuelewa maneno yote ambayo yanatamkwa na wanawake. Lakini ukweli ni kuwa ni chini ya asilimia 20% ambayo wanawake wanasema ambayo wanaume wanaweza kuelewa.



Ok twaweza kusema kiujumla kuwa wanawake ni kama viumbe ambao wanatoka katika sayari nyingine kwa mtazamo wa mwanaume yeyote.

Lakini kuweza kuwaelewa wanawake angalau kwa asilimia 50% utafanyaje?

Soma miondoko yake ya mwili aka body language:
1. Jinsi wanavyojitandaza
2. Vile mapozi yao yako
3. Jinsi 'wanavyoitumia' miili yao kwa ujumla

Kwa mwanaume yeyote ambaye yuko serious kutaka kutongoza mwanamke yeyote, lazima awe na ujuzi wa kuisoma miondoko muhimu ya mwanamke ambayo inaashiria iwapo amevutiwa kwako au la.

Katika kufafanua zaidi, post hii tumeiandaa specially kuonyesha iwapo mwanamke anakupenda au la kwa kuangalia sehemu moja kuu kutoka kwake....

Zama nami...

Kuangalia miguu ya mwanamke kama anakupenda au la

Ni rahisi kudhibiti vile sura yako unataka ionekane. Kwa kutumia uso unaweza kuleta mitazamo tofauti kabisa na vile ambavyo unajihisi. Sura yako inaweza kushawishi kwa kudanganya, kutabasamu mbele ya kamera nk. Hata hivyo, kadri unaposongea mbali na uso wako, inazidi kuwa vigumu kuudhibiti mwili wako kwa ujumla.
Hii ni kumaanisha kuwa miguu (nyayo) ni kiungo muhimu cha kutumika kung'amua maswala ya kuvutiwa kimapenzi katika mwili wako mzima.
Halafu uzuri wake ni kuwa ni rahisi kuichambua. Kimsingi ni kuwa kila mtu hutumia miguu yake kuelekeza kitu ambacho anapendezwa nacho. So, iwapo unadhania ya kuwa unazungumza mazungumzo yanayovutia na mtu kwa kuwa anatabasamu na kucheka...
...halafu uje ugundue ya kuwa miguu yake hailengi kwako bali kwa mlango wa nje ...utajua ya kuwa hautakikani hapo.
Binadamu hutumia miguu yao kama vile wanavyotumia mabango ya ishara kuelekeza kitu ambacho wanataka. Sheria hii unaweza kuitumia vizuri katika maswala ya kudeti na kutangamana na wengine.
Wataka kujua kama mwanamke amevutiwa na kupendezwa kwako?
Fanya kuiangalia miguu yake mnapoongea. Miguu ambayo inalenga upande wako ni ishara dhabiti kuwa anapendezwa na wewe (kama hatakuwa akiisongeza mara kwa mara)
Vile vile, kama mguu wake ama miguu yake inalenga kwingine ama atakuwa akichezacheza na viwiko vyake vya mguu ni ishara ya kuwa hajapendezwa nawe, ama anataka kuondoka hapo mara moja.

Upo!? [Soma: Siri zilizofichwa jinsi ya kumvutia mwanamke]


Sababu 3 Kuu Ambazo Zinakufanya Ushindwe Kumtoa Mwanamke Deti

Acha tuwe waadilifu kiasi...

Baadhi ya wengine wetu  wanashindwa kupata deti na mwanamke.

Baadhi ya wengine wetu wanaweza kupata deti mara ya kwanza lakini wanashindwa kupata deti ya pili.

Wengi wanadhania ya kuwa si makosa yao - eti ni makosa ya mwanamke mwenyewe.

"Nilimwita tukatoka deti mara ya kwanza, nilipomwambia tutoke deti ya pili alikataa. Sijui tatizo liko wapi"

So tatizo huwa linajitokeza wapi?



Kulingana na tafiti tulioufanya katika blog hii, tumekuja na sababu tatu kuu ambazo zinachangia wengi kushindwa kutoka deti na mwanamke mara ya kwanza au mara ya pili.

#1. Haujitayarishi kutengeneza deti ya pili wakati ambapo deti ya kwanza bado haijakamilika. Pia itakuwa hujamsisimua vizuri kuhusu wakati ambapo mtakutana tena katika deti ya pili.

Ok mpango mzima huwa hivi, iwapo unataka deti ya pili na mwanamke itendeke, lazima umwelezee na mapema kuhusu deti yenu ya pili. Pia iwapo unataka deti ya pili na mwanamke lazima umsisimue kuhusu deti yenu ya pili, mfano unaweza kumdokezea kuhusu mambo ambayo unatarajia kumfanyia mtakapo kutana mara ya pili nk.

#2. Itakuwa haujitahidi kuwa wewe mwenyewe. Itakuwa unababaika na kuwa na wasiwasi wa kutaka kuhakikisha ya kuwa husambaratishi deti yako naye, jambo ambapo linafanya deti yako na mwanamke kuharibika.

Kwa kawaida mwanamke hupenda mwanaume ambayo yuko wazi, mwenye nishati na pia hisia. Hivyo ni rahisi sana kwa mwanamke kutambua iwapo mwanaume ameingiwa na wasiwasi ama uoga.

#3. Hausikilizi kile ambacho anasema. Tatizo hili humkumba mwanaume wakati ambapo anajaribu kufikiria sana kuhusu mambo ambayo anataka kumuuliza ama kumjibu mwanamke ili kutafuta vitu mnavyohusiana pamoja badala ya kumakinika na kumsikiliza mambo ambayo anayasema.

Ok... kwa kifupi ni kuwa hizi sababu tulizozieleza hapo juu huchangia kwa mwanaume kushindwa kuzuia deti kwa mara ya kwanza kwa mwanamke au kwa mara ya pili.

Kama umetoka deti na mwanamke kwa mara ya kwanza, sioni tatizo la kwako kushindwa kutoka naye deti mara ya pili, tatu, nne na hata ya tano na mwanamke unayemfukuzia.

Kile unachopaswa kuzingatia ni kuangalia vile ambavyo unawatendea katika deti, ujanja wako wa kutumia mbinu kadha wa kadha za kuwashawishi, na cha msingi ni vile ambayo utamakinika kutaka kujua vitu ambavyo mwanamke anataka katika deti.

Mbinu Asilia Ya Kutumia Kumfanya Mwanamke Akupende

Kila mtu hupenda mambo yafanyike haraka haraka.

Awali tuliweka chapisho la kutumia saikolojia marufuku kumtongoza mwanamke na ilipendwa sana na masomaji wetu, kando na kuwa ilikuwa trending topic kwa muda mrefu.

Swali sasa ni: Je, kuna mbinu asilia ya kutongoza mwanamke?

Nauliza hivi kwa sababu baadhi ya readers wetu kando na kujua kutumia saikolojia, wangependa pia kuijua mbinu asilia ya kumpendeza mwanamke. Well, jibu ni NDIO.

Kama paneli ya NESIMAPENZI, tumeamua kuiandaa mbinu hii ambayo kwa kawaida hutumika sana na wanaume wengi bila wao kuitambua, ama kuitumia vibaya.

Zama nami!


Mbinu asilia ya kumfanya mwanamke akupende

1. Kuwa tofauti
Hii ni mbinu muhimu zaidi ambayo unafaa kuiweka viganjani mwako. Kama wataka mwanamke yeyote, basi unapaswa uwe tofauti na wanaume wale wengine wote ambao wanamfukuzia.
Itakusaidia zaidi kama utafanya utafiti wa kina kwa mwanamke aina hii. Lazima ujue mambo ambayo anayapenda maishani mwake. Mfahamu vizuri kama ni mwanamke anayependa kujua mambo mapya ama ni mwanamke mwenye aibu. Pia mfahamu kama ni mwanamke anayependa kutangamana na watu ama ni wale wapole. Kimsingi hakikisha unafanya utafiti wa ndani zaidi kumhusu ili hio siku mtakutana ama unapoongea naye hatoboeka na wewe.
Kulingana na wanasayansi, wanawake huvutiwa sana na rangi nyekundu
Kama utaamua kutofanya utafiti wowote kumhusu na ukaamua kwenda direct moja kwa moja kwake, basi fahamu ya kuwa wanawake hawapendi wanaume ambao wanaboesha, na ambao wanatabirika kirahisi. Ok. Mbona usijaribu kuvalia nguo ya rangi nyekundu? Yeah. Kulingana na utafiti wa kisayansi, wanawake huvutiwa sana na wanaume ambao huvalia rangi nyekundu. Wanawake hupendezwa na wanaume tofauti na wenye kuvutia.
Kumbuka- si lazima uoekane bora zaidi; bali tofauti.
2. Mwonekano wako
Tofauti na tamaduni za tangu jadi, si lazima mwanamke apendezwe na mwanaume mrembo wa kuvutia ndipo atoke deti na yeye. Ijapokuwa kuvutia na kuwa na miraba minane ni nyongeza katika sekta ya dunia ya kudeti, si muhimu sana kama inavyopigiwa kamsa. Vivyo hivyo, ni muhimu sana kama utaubadilisha mwonekano wako ili uweze kumvutia mwanamke unayeazimia kumfukuzia. [Soma: Mbinu za haraka za kuujeuza mwonekano wako]
3. Jenga uzingiti wa hisia
Kama wataka kujua njia rahisi ya kumfanya mwanamke akupende kwa uharaka, jenga uzingiti wa hisia na yeye (ok. wengi wanaogopa mbinu hii kwa kuwa ni rahisi kuwekwa katika kategoria ya friend zone) lakini kama utamfanya mwanamke kuwa rafiki yako kabla kumwambia azma yako, utakuwa na nafasi kubwa ya kumjua ndani na nje na kila kitu kumhusu, kutumia muda wako mwingi na yeye na pia kumfanya ajiskie huru akiwa na wewe. Bydaway nani hajui kama rafiki yako anapaswa kuwa mpenzi wako? [Soma: Sababu za lazima unafaa kufanya mapenzi na rafiki yako]
4. Ongea (tumia viini macho)
Kwa kawaida huwa ni vizuri zaidi iwapo utaanza approach ya kwanza kumtongoza mwanamke unayemzimia kabla ya yeye kuchukua hatua. Pia ni vizuri kujua mada ambazo zitamfanya yeye kukupenda bila ya yeye kuelewa ni kwa nini. Maongezi yako hapa unafaa kuyafanya ya KUZIMU na pia matumizi ya maongezi ya viini macho. [Soma: Matumizi ya viini macho kumsuka mwanamke]
5. Kuwa Juma Nature
Wanawake wengi wangependa kudeti mwanaume ambaye anamaisha yake binafsi kando na dunia ya kudeti. So iwapo utamwonyesha mwanamke ya kuwa wewe una kazi zako nyingi binafsi wakati wako wa uhuru utamwashiria mwanamke ya kuwa hutaambata kwake na hutotaka kuutumia muda wake mwingi kwako. Pia hii itaashiria ya kuwa umekomaa na una maamuzi na malengo yako binafsi maishani na kuwa si rahisi kwako kumuacha.
6. Tangamana
Wanawake wengi huwa wanapenda kutangamana, hivyo itasaidia pakubwa iwapo pia wewe unapenda kutangamana. Mwanzo uzuri wa kutangamana ni kuonyesha ishara kwa mwanamke ya kuwa maisha yako hayaboeshi hivyo itakuwa rahisi kwa mwanamke kukupenda. Usione haya ama aibu, tangamana na marafiki zake, familia yake ili upate kuwajua zaidi na pia kukupa alama za ziada za kupendekezwa. [Soma: Jinsi ya kujifundisha kukutana na wanawake wapya]
Mwisho ni lazima ujue mbinu tofauti tofauti za kunoa makali yako ya kumfanya mwanamke akupende. Posts nyingi humu ndani zitakupa mwongozo wa wewe kufanisha azma yako kwa urahisi sana.

Jinsi Ya Kuonyesha Kuwa Una Hadhi Ya Juu Kwa Mwanamke

Ushawahi kugundua ya kuwa wanawake kikawaida huvutiwa na wanaume ambao wana hadhi ya juu? Kama ni kweli, najua kwa akili yako unafikiria ya kuwa iwapo unataka kuwavutia wanawake warembo lazima uwe na umaarufu ama tajiri ama zote mbili. Ni kweli?



Ok hapa NESIMAPENZI tunasema La! Unaweza kumwonyesha mwanamke kuwa pia wewe una hadhi ya juu....na si lazima uwe na pesa nyingi wala kuwa staa wa Bongomovies...

Mwanzo kuwa na hadhi ya juu ni nini? Je, kuwa mtu wa hadhi ya juu ina maanisha kuwa tajiri ama maarufu? Ok hebu fikiria hivi: Kama mtu tajiri zaidi ulimwenguni ameamua kusafiri hadi kisiwa flani kisichojulikana ambacho hakina runinga wala redio... mtu huyu atakuwa na umaarufu kiasi gani? Pesa ambazo anazimiliki zitakuwa na umuhimu gani?

Ni hivi, kuwa na hadhi ya juu ni mauzauza. Ni mauzauza ambayo yanajengwa na maoni ya watu ambao unahusiana nao karibu. Mfano, unaweza kuwa na hadhi ya juu ya maingiliano wakati ambapo unatangamana na familia yako, tofauti na kuwa katika chumba ambacho kimejaa watu ambao huwafahamu.

Hivyo kama unataka kuonyesha hadhi ya juu kwa mtu flani, kuna mbinu mbili ambazo unaweza kutumia...

Kwanza: Nufaika na koti ya nyumbani
Katika michezo, kunufaika na koti ya nyumbani inamaanisha kuwa una nambari kubwa ya mashabiki ambao watakupa sapoti na ambao wanayaelewa mazingira uliyomo. Hivyo unaweza kutumia mbinu hii katika maisha yako ya kujamiiana na watu kwa kuchagua sehemu mahususi ambazo utakuwa 'mtu wa kawaida' katika hizo sehemu.

Kwa mfano, kuwa mtu wa kawaida katika baa ama klabu ina maana kwamba unaenda sehemu hizo mara kwa mara, na pia wafanya kazi wote katika sehemu hizo wamekuzoea mpaka wanakujua kwa jina. Kwa ufupi ni kuwa umepandisha hadhi yako ya kujamiiana na wengine katika sehemu hizo kwa sababu unaonekana sehemu hizo mara kwa mara.

Fikiria hili jambo wakati mwingine ambapo utahudhuria sehemu nyingine ambayo hujawahi kuitembelea hata mara moja. Ni tofauti gani ambayo utaihisi iwapo umekuwa ukiitembea sehemu hio kwa miaka mitatu iliyopita? Je si ingekuwa rahisi sana kuwaonyesha wanawake waliokuzunguka kuwa wewe ni mtu wa hadhi ya juu?

Bila shaka ingekuwa... mwanzo kama mwanamke mwenyewe si mtu wa kawaida katika hio sehemu! Ungemtembeza sehemu hio na kumtambulisha kwa "marafiki" zako wafanya kazi pamoja na wateja uliowazoea wa kawaida.

NB: Nenda utafute sehemu mbili ama tatu ambazo utakuwa mtu wa kawaida katika sehemu hizo. Hakikisha ya kuwa sehemu hizo ni ambazo zina wanawake wengi ambao wanaweza kustahili kuwachagua.

Pili: Jenga uhusiano mwema na koti ya nyumbani
Pindi ambapo ushatambulisha sehemu zako ambazo zitakuwa "manufaa ya koti-nyumbani", anza kujenga uhusiano mwema na watu ambao wanakuwa hapo wakati mwingi. Sehemu nzuri ya kuanza ni kwa wafanya kazi, kwa kuwa kila wakati huwa hapo na mara nyingi huwa jamili.

Jifunze majina ya watu na angalau ujue jambo moja linalowavutia. Hakikisha ya kuwa unakuwa mkunjufu kwa wafanya kazi na pia kuwapa bahshishi mara moja au nyingine. Pia usisahau kutambulisha majina ya wafanya kazi wengine iwapo utakumbana na wafanya kazi wengine wapya.

Hii itasaidia kugundua ya kuwa wewe ni mtu ambaye unajulikana na wafanya kazi wale wengine, na itasaidia kuonyesha hadhi kuu kwako kwao.  Fanya mazoezi ya mara kwa mara na uwe na subira, na uanze pia kutangamana na wateja wa kawaida katika sehemu hizo.

Kwa muda wa wiki kidogo, itakuwa rahisi kwako kumuonyesha mwanamke yeyote ambaye unakutana naye kuwa wewe ni mwanaume wa hadhi ya juu katika sehemu hizo.

Upo!?

Siri 4 Zinazofichwa Za Jinsi Ya Kumvutia Mwanamke

Kuna mbinu nyingine za kumvutia mwanamke ambazo haziwekwi hadharani kwa kila mtu kuzijua. Na hata kama ulikuwa ukizijua ni kuwa ulikuwa hutambua manufaa yake kwako hivyo ulikuwa ukizitumia vibaya. Mfano leo kama ungekuwa unazijua mbinu zote mwafaka za kumfanya mwanamke atamani kila kitu kutoka kwako si ingekuwa balaa?



Post ya leo tumeamua kukuandalia mbinu ambazo ukizitumia vizuri bila shaka itakuwa ufunguo wa kwako kuweza kulazwa na mwanamke yeyote yule.

Zama nami!

Siri za kumfanya mwanamke akupende

1. Kuwa na hadhi ya juu kijamii
Ushawahi kugundua vile watu matajiri na watu wenye hadhi ya juu huwa na maongezi na swaga ambazo huonyesha mamlaka? Watu aina hii huonyesha dhamana na hadhi ya juu kiasi cha kuwa hawaogopi kuonyesha hisia zao kwa mwanamke wala kuingiwa na wasiwasi wa kuwa wanaweza kukataliwa.
Wakati mwanamke anapokutana na mwanaume mara ya kwanza, hapo hapo hutoa uamuzi akilini mwake iwapo atalala na yeye au la. Kiujumla, haswa kwa wanawake warembo, huwa na nadhari iliyojengwa akilini mwao kwa vitu wanavyothamini. Vile ambavyo atakavyokukufikiria ndivyo atakavyokuchukulia kama thamani yake kwako. 
Kiufupi ni kuwa, wanawake huvutiwa na wanaume ambao wamepita thamani yao ambayo wamejiwekea. Hapa ndipo unapofaa kutumua nguvu za kijamii kukuongezea hadhi yako katika jamii.

Kuna njia tofauti tofauti za kufanilisha hivi. Njia rahisi ni kuhakikisha ya kuwa watu wanakuzungumzia na kuongea kuhusu mambo ambayo umefanikiwa kufanya ama kutimiza. [Soma: Jinsi ya kuipandisha hadhi yako kwa mwanamke]

2. Ujuzi wa kuwasiliana
Ok. Ushaongea na mwanamke kwa njia ya kumridhisha bila kuchekwa. Kila kitu kinaenda sambamba mpaka inafikia mahali flani unaishiwa na maneno ya kumwambia.

Ghafla, unamwona akikuangalia kwa matumaini, akitaka uendeleze na gumzo lakini unashindwa. Unabakia ukijiuma midomo na kujikuna kichwa huku ukimwona mwanamke aina hii akikutoka viganjani mwako na kuchukuliwa na mwanaume mwingine aliekaa pembeni. Situation kama hii inaumiza bila shaka.

Sababu kuu ambayo inawafanya wanaume wengi washindwe kuongea na wanawake ni kuwa wanaishiwa na mawazo ya kuongea. Ni muhimu kukumbuka ya kuwa katika mchezo wa kutongoza maongezi yako ni kama bango la mauzo kwa mwanamke. Hii ni kumaanisha kuwa kando na kuwa unajua kile ambacho unaongea, unafaa ujue jinsi ya kumudu na kuendeleza mazungumzo mazima.

Wakati unapomsuka mwanamke una muda mchache kabisa wakujifanyia mauzo. Hivyo ni muhimu zaidi upange hoja zako vile ipasavyo ili mwanamke akitoka hapo asiweze kukusahau kiurahisi. Na kufanikiwa kuujua ujuzi kama huu hauwezi kuja na siku moja, lazima ufanye mazoezi ya mara kwa mara mpaka ujeuke gwiji.

Kuongea na watu tofauti tofauti kutakusaidia kujenga confidence ambayo itakurahisishia kuongea na mwanamke wakati ambapo utakumbana naye. [Soma: Jinsi ya kuongeza ujuzi wa kuwasiliana]

3.Kuidhibiti miondoko ya mwili
Kulingana na utafiti wa kisayansi, binadamu huwasiliana asilimia 93 wakitumia miili yao na asilimia 7 kwa kutumia maneno. Ni muhimu kumakinika na kuelewa miondoko yako yote wakati ambapo unazungumza na yeyote yule.
Jitenge na tabia ya kuikunja mikono yako ama kujikunja kunja kwa sababu hio ni ishara ya kumwambia mwanamke akuondokee ukae pekeako. Na ukiendelea na tabia kama hii itakiwa kitu cha kwanza ambacho atakinotice wakati mumetoka deti.

Badala yake, tumia miondoko ya mwili ambayo inafahamika na kila mtu. Mfano ni kuegemea mbele wakati ambapo unaongea, kuifumbua mikono yako na pia kuweka pozi ambalo linaashiria kupumzika. [Soma: Matumizi tofauti ya miondoko ya mwili]

4. Kufanikiwa kiubora
Si jambo la kushangaza kwa wanawake kuwaona wanaume ambao wana ubora flani katika nyaja kama vile muziki, michezo, sanaa nk kuvutia kwa hali ya juu. Wanaume aina hii huwa wamejikuza na stadi zao kiasi cha kuwa wamebobea kwayo.

Ok tunajua ya kuwa ni kweli hauwezi kuwa mtajika kama vile Emmanuel Adebayor, lakini unaweza kutajika kwa maswala madogo madogo katika fani flani unayoipenda. Labda wewe ni bingwa mtajika katika gemu ya karata ama labda wewe ni kapteni wa timu yako ya raga nk.

Kulingana na shauku yako yeyote unayopenda, unaweza kumjulisha mwanamke kimtindo flani bila kujifanya kana kwamba unajipa sifa kujipendekezea. [Soma: Mambo hupaswi kumwambia mwanamke]


La mwisho ni kuwa hizi ni baadhi ya mbinu ambazo unafaa kuzijua na kutimiza kama unatumaini kuwa na mafanikio ya juu kwa mwanamke.

Jinsi Ya Kuyafanya Maongezi Yako Na Mwanamke Yawe Marefu

e kuna kitu ambacho kinafurahisha zaidi (kando na kufanya mapenzi) ambacho kinasisimua zaidi kuliko kuwa na mazungumzo ya kufurahisha na mwanamke? Ok. unajua vile mazungumzo aina hii hutokea, wakati ambapo unayaona mazungumzo yako na mwanamke yanaenda na wimbi moja, unajihisi kana kwamba mko mkondo mmoja, na cha kufurahisha zaidi ni kuona ya kuwa mnamaliziana sentensi zenu bila wasiwasi halafu...



Ghafla inatokea situation ambayo kuna kuwa na kimya. Wakati ambapo umebakia unang'ang'ana angalau upate kitu cha kufanya maongezi yenu yarudie tena , kuna ile hisia ya pole pole inayokuja ambayo unajihisi kana kwamba unapoteza nafasi yako na mwanamke huyo kuendeleza matangamano yenu. Kibaya zaidi ni kuwa, kadri kimya kinapoendelea kuzidi...ndipo unazidi kuwa na mawazo ambayo hayana msingi ambayo unayajaribu kuyasema.

"So, anga ya leo unaionaje?" ama "leo kuna jua kali!" ni maneno ambayo unabakiwa nayo kuyasema ukijaribu angalau ufanye ukimya wenu upotee...

Well, kama umekuwa ukikumbwa na changamoto kama hizi wakati ambapo unajaribu kuongea na mwanamke... acha tuongee jinsi ya kuhakikisha ya kuwa unakwepa jangamizi hili wakati ambapo unakuwa na mwanamke.

1. Usipange kuhusu maongezi yako ya mbeleni sana... lakini...
Ingawa itakuwa ni jambo mwafaka la kupanga kitu cha kusema mbeleni wakati ambapo unakumbwa na hisia za shoto (awkward), hii inaweza kufanya kutangamana kwenu kuonekana shoto zaidi. Walakin kuna njia kadhaa ambazo unaweza kusema wakati ambapo unakumbwa na kimya kirefu. Maneno haya yatasaidia sana haswa wakati imetokea situation kama hii.

Hizi ni baadhi ya sentensi unaweza kutumia wakati kimya kimewajia ghafla katika maongezi yenu:

"Ushawahi kujiuliza ni kitu gani kinachofanya kimya kirefu kuleta hisia za shoto?"

Ukifikiria vizuri kuhusu hili swali, utaliona kuwa ni swali zuri ambalo linasisimua na ambalo linaweza kujenga maongezi marefu. Swali kama hili pia linakupa wewe nafasi ya kuweza kupata kuijua haiba ya mwanamke unayeongea naye.

"Ulikuwa wajua ni njia gani rahisi ya kuonyesha kuwa unamtambua na kumfahamu mtu flani? ---mpe nafasi akujibu--- "Wakati ambapo inatokea ukimya wenu mumeuzoea kuwa ni sehemu yenu ya mazungumzo.  Je, uligundua hilo?"

Hii tena inatoa nafasi kwako kupata kumwelewa zaidi mwanamke unayeongea naye na bila shaka inaweza kumfanya mwanamke kuvutiwa kwa mazungumzo ambayo utakuwa ukiyaendeleza. Kutumia mbinu hizi pia kunasaidia kufanya ukimya wenu kuonekana kama kitu ama jambo la kawaida bila kuleta  hisia za shoto. Hii ni kwa sababu mambo ambayo huonekana kama hayajazoeleka yakiwekwa wazi na kuzungumziwa kwayo inayafanya yaonekane kama mambo ya kawaida.

Hii ni kweli kwa sababu hisia za shoto ambazo zinajitokeza katika maongezi ni sawa na jambo lolote lile ambalo huonekana kama ni geni. Lakini pindi ambapo mtaamua kuweka wazi na kuliongea swala hilo, inatoa hisia zozote ambazo zinaweza kuharibu maongezi yenu.

NB: Anza mazoezi ya kutumia mbinu hii kwa kuwauliza marafiki zako na watu unaotangamana nao kabla ile siku ya kuanza kuongea na deti wako. [Soma: Mada ambazo zitaua upendo kwa mwanamke]

2. Mtie ufunguo yeye ndie awe anayeongea
Wanaume wamebarikiwa sana kwa kuwa wanawake ndio wamepewa talanta ya kuongea. So kwa mwanaume akicheza karata zake vizuri, hahitaji kufanya mengi ikija kwa maswala ya maongezi. Kile kinachohitajika ni kujua wakati na maswali ambayo unafaa kumuuliza mwanamke na kuwa msikilizi mzuri.

Ukiwa mbora zaidi wa kusikiliza anachosema ndipo unapomfanya azidi kuwa interested na kuongea na wewe. Pia utakuwa ukimfanya ajiskie huru kwako. Mwanzo iwapo utamfanya ajihisi yuko huru kwako utafanya maongezi yenu yawe marefu zaidi kuzidi yale ambayo ulikuwa ukiyatarajia.

Ufunguo hapa ni kujua jinsi ya kuyaandaa maswali yako kulingana na kitu ambacho anaongea. Kama anakuambia kuhusu kitu anachopenda, muulize kwa nini anakipenda. Kama ni kitu asichokipenda, muulize kwa nini hakipendi.

Kuuliza swali la 'kwa nini' huwa inasaidia sana kuingia katika mzizi wa haiba  yake na kutakufanya umuelewe kiundani zaidi kumhusu. Kadri unapozidi kufanya hivi, ndipo unazidi kumfanya afunguke na kuongea vitu zaidi ambavyo utakuwa na nafasi ya kuuliza maswali zaidi kwayo.

Kando na hio usijisahau ukaingia katika wingu la wanaume wengine wengi feki ambao hupenda kujibu maswali na neno moja. Ni muhimu kuhakikisha ya kuwa wakati ambapo yeye pia atakuuliza swali uhakikishe ya kuwa unafunguka na kuelezea kila kitu ambacho unaona kinafaa kwa yeye kujua.

Kawaida ni kuwa kadri unapofunguka kujieleza kwa mwingine, ndipo pia yeye anafunguka kukuelezea yake...na hii huchangia mazungumzo yenu kuwa wazi na marefu. [Soma: Jinsi ya kuongea na mwanamke umvutie]

SMS Za Nguvu Za Kutumia Baada Ya Kupewa Namba Na Mwanamke

angu tuweke chapisho ambalo linagusia swala la mbinu tofauti tofauti za kuomba namba ya simu ya mwanamke, tumekabiliwa na janga jingine ambalo baadhi wa readers humu ndani wamekuwa wakituandama katika inbox na maswali ya kurudia rudia ya 'Jinsi ya kuufunga mchezo baada ya kupewa namba na mwanamke'

Tumekuwa tukiwajibu baadhi ya readers wetu na tumeamua kuweka wazi mbinu rahisi ambayo itamfunga mwanamke ili uweze kukutana naye mara ya pili, ya tatu, ya nne...

Na kufanikisha hivi, tumekuja na mbinu ambayo kwa kawaida imekuwa ikitumiwa na guru wengi ambao wamebobea katika sekta ya kudeti wanawake.

Zama nami...



Ok. Umefuata mbinu ya moja kwa moja ukamfanya mwanamke akakupatia namba yake ya simu.

Uliongea naye na uliona anavutia kupindukia...

Ulikuwa ama alikuwa na haraka hivyo hukupata nafasi ya kuongea naye kwa muda mrefu bali ulichukua namba yake ya simu.

Sahizi umeachwa hujui ufanye nini!

Je umpigie simu ama umtumie ujumbe mfupi?

Utasema ama utamwambia nini baada ya kuwasiliana naye?

Je, utamuuliza kama atoke deti na wewe au la?

Ok bila kupanic, mbinu ya kufanikisha maswali haya ni rahisi...

Mwanzo ni rahisi kama kusema A...B...C...

SMS za nguvu za kumtumia mwanamke siku ya leo baada ya kukupatia namba

1. Funga deti na yeye 
Jambo la kwanza kabisa ambalo unafaa kufanya wakati ambapo atakuachia namba yake ya simu ni uhakikishe ya kuwa unamwomba atoke deti na wewe. Na meseji unayohitajika kumtumia ni kama ifuatayo...

"Hi. nlikuwa nahakikisha kama umefika nyumbani salama. Nimefurahia sana kukutana na wewe. Ningependa tukutane wakati mwingine. Jumamosi nitakuwa free. Nije nikuchukue wakati gani?"

SMS hii huwa inafanya kazi kwa mambo mawili: Jambo na kwanza ni kuwa inamfanya ajihisi yuko salama, yani kujiona ya kuwa kuna mtu anadhamini maslahi yake, jambo ambalo wanawake wengi wanatamani kuwa nalo.

Pili ni kuwa unamlazimisha kujiazima. Aidha akubali kutoka deti na wewe ama kukukataa papo hapo. Kivyovyote vile utaujua msimamo wake.

Kama atakubaliana na wewe na kujibu sms yako,  turuke katika hatua ya pili.

2. Mfunge kwa kumpigia simu
Kabla kutoka deti na yeye lazima ufahamu mambo angalau kidogo kumhusu. Kujua mambo kadhaa kumhusu kutakupa wewe nafasi ya rahisi kuifanya deti yako na yeye kuvutia, bila kuboesha. Pia kumpigia simu kunajenga ile hisia ya mapenzi ambayo hujitokeza katika mazungumzo ya simu.

Pia unataka kumjulisha ya kuwa uko interested na yeye, lakini usiivuke mipaka yako hapa. Meseji ya pili inafaa ienda hivi:

"Poa. Natumai kukutana na wewe hio siku. Nitakupigia simu wakati flani kukujulisha vile tutavyoendelea. Kesho inaweza kuwa siku nzuri kwako?"

 Kutumia meseji hii ina nguvu zifuatazo:  Unaufunga mchezo wako wa simu. Unamwambia ya kuwa deti yenu itafanikiwa. Pia unamwambia ya kuwa unapanga sehemu ambayo unapania kukutana kwa deti. Kiukweli ni kuwa utajua vitu ambayo anapenda wakati ambapo utampigia simu, na hii itakuwa kama msingi wenu wa kwanza katika deti.

Halafu sasa itambidi akujibu. Na hapa ndipo maongezi yenu yataanza kupanda kwa kasi. Haswa kama amependezwa na wewe.

Mwanzo meseji ambazo atakuwa akituma baada ya hizi mbili kutaashiria kwako kuweza kutoka deti na yeye mara kwa mara...na hata kufanya kufikia level ya texts za kimapenzi.

Upo!? [Soma: Hatua za kufanya kama mwanamke hataki kujibu texts zako]

Jinsi Ya Kumuathiri Mwanamke Na Mbinu Ya 'Wazo Mkato'

magine unaaproach mwanamke wa ndoto yako, halafu sahizi unaongea naye. Kwa kuwa unataka kumfanya akuwe interest na wewe muda wote unatumia mbinu zifuatazo kuhakikisha anapendezwa nawe...

Je, uli...

- mwambia stori ya kupendeza kuonyesha kuwa una 'hadhi ya juu'

- fanya maujanja ya kiini macho ili umfurahishe...

- buni maslahi ya uongo (interest) halafu ukamwambia ajieleze kwa undani huku ukihakikisha kwa kujifanya ya kuwa unamsikiliza kwa umakini...

...na orodha ni ndefu haiishi na hapo...



Kwa mshangao kwako unamwona akiangalia juu ya bega lako mara kwa mara, na anaonekana kuwa amevutiwa na mambo ambayo yanafanyika kando yake (isipokuwa wewe). Unaanza kujishuku na uwezo wako wa michongo ya kuhifadhi, na kutojiamini kunaanza kugonga katika akili yako.

Unajaribu kumaintain hadhi yake ya maslahi, lakini unagongwa na jibu, "Nimefurahi kukutana na wewe, lakini nataka kuondoka sahizi".

Ok relax. Usibabaike. Sote tumeshawahi kuwa huko wakati flani. Pia mimi nishawahi kupatikana.


Wakati ambapo imekutokea, najua ulikuwa na mawazo ambayo yalikuwa yakikugonga kichwa. -"Kama tu ningekuwa na uwezo wa kumwambia stori za kuvutia zaidi, najua angevutiwa na mimi zaidi na zaidi."

Ndio nakubali hii ingekuwa ni ukweli (kwa kiasi flani), lakini kuna vitu unafaa kujua kwanza-


Kile UTAKACHOSEMA si muhimu na vile ambavyo UTAKAVYOSEMA.

Kwa sababu hii, chapisho hili kutoka kwangu sitakufundisha jinsi ya kujifunza kutumia mistari ya papo kwa hapo, michongo, mbinu murwa za kumfurahisha wala mbinu za kumchekesha mwanamke.


Badala yake, utavumbua SIRI MOJA ya kumnasa mwanamke ambayo hujawahi kuiskia wala kuisoma mahala popote pale. Kwa kutumia mbinu hii ambayo nimeamua kugawa nawe, utakuwa na uwezo wa kumfanya mwanamke yeyote kuendelea kuwa interested na wewe -bila kutilia maanani kile ambacho utasema.

Shuleni, ulifundishwa ya kuwa unapaswa kumaliza hoja fulani kabla ya kuenda kwa hoja ama mada nyingine. Kwa ukweli, huu ulikuwa ni ushauri mzuri, lakini tu kama unataka kumfanya mwanamke alale.


Iwapo unataka kuwa kama Don Juan na kuwafanya wanawake wakuwaze ndotoni mwao, basi unafaa uache hii tabia na uanze kutumia mbinu ambayo nataka kukuonyesha sasa hivi.

Mbinu Ya 'Wazo Mkato' - Ni nini, Na Kwa Nini Inafanya Kazi

Mbinu ya 'wazo mkato' ni rahisi kuieleza, kama tu vile jina lenyewe linavyomaanisha - ni mawazo au stori ambayo haijakamilika. Unaanzisha stori ya kuvutia, halafu badala ya kuimaliza, unaanzisha stori mpya.


Wakati ambapo tunakumbana na wazo ambalo halijakamilika, akili zetu zinalazimishwa kutafuta jinsi ya kutatua jambo hilo. Kwa mazingira ya kuwavutia wanawake, mbinu ya 'wazo mkato' inamlazimisha mwanamke kumakinika na kila ambacho utakuwa unasema - hii ni kwa sababu akili yake haitomruhusu kufanya jambo jingine.

Hebu fikiria unamwendea mwanamke na kumwambia, "Hi. Naitwa Papito, na mimi ni mweka hazina katika Benki ya Barclays. Unataka kujua nimefanya kazi gani siku ya leo?"

Nafasi hapa ni kuwa hatakuwa na interest zozote kutaka kujua kutoka kwako -hii ni kwa sababu umejitokeza kama mtu ambaye hana thamana ya kuongea naye kamwe.


Badala yake mbona usimwambie "Kuna kitu ambacho nakijua kukuhusu, lakini siwezi kukuambia." Hii itajenga tenshen katika akili yake -ambayo inaweza kutatuliwa na wewe pekee.

Hapa gundua ya kuwa nishati zote zimelenga KWAKO. Wewe sasa ndiwe utakayethibiti maongezi na kutangamana kwenu, na utagundua ya kuwa CHOCHOTE utakachomwambia (kuanzia mwanzo hadi mwisho) atakumbuka.

Nishati ya nguvu! Ama waonaje?

Jinsi ya kutumia mbinu hii wakati mwingine ambapo utakutana na mwanamke usiyemjua

Wakati ambapo unakutana na mwanamke, je huwa unamwambia jina lako ghafla wakati ambapo unamsalimia kwa kumpa mkono? Kama ni kweli, basi kuna nafasi kuu kuwa atasahau jina lako (ama kitu chochote kukuhusu) wakati ambapo atamaliza maongezi na kuenda zake.


Hivi ndivyo ambavyo ninavyosema wakati ambapo mwanamke ananiuliza jina langu - kwa kutumia mbinu hii ya 'wazo mkato'.

"Babangu alikuwa anapenda kuniambia ya kuwa mwanzoni alitaka kuniita jina la Abujahal - baada ya amiri jeshi mkuu wa Rashidun enzi za zamani. Halafu nilimuuliza, "baba, hilo ni jina zuri kabisa. Mbona hukuliweka?"
Na aliniambia hivi, "Ok. Sababu kuu ni kuwa kulikuwa na samaki ambaye tulikuwa tukimfuga alikuwa pia anaitwa Abujahal, na ile siku ambayo ulizaliwa aliweza kuliwa na paka ambaye tulikuwa tukimfuga ambaye aliitwa Muadh. So hatukutaka kukumbushwa kuhusu huyo samaki aliyekufa so tukaamua kukuita Ibrahim""

Badala ya kumwambia jina langu hapo hapo, huwa nimezunguka katika mada kuhusu jina langu, na hivyo kuibua maswala ambayo yanakuwa kama tenshen katika akili yake.

Bila kujielewa atajaribu kuvumbua tenshen hio, hivyo kumfanya aathirike zaidi na kila neno ambalo litatoka kutoka kwa kinywa changu.

Kama ningemwambia direct kuwa naitwa 'Ibrahim Morowa' kuanzia mwanzo, angekuwa ashanihukumu kama wanaume wale wengine ambao amekutana nao katika party flani, na hangenitambua.

Kwa kutumia mbinu hii ya 'wazo mkato' nimeonyesha mambo matatu makuu wakati mmoja: kwanza ni kuwa nina hadhi ya juu, pili ni kuwa nina hisia ya juu ya ucheshi, na tatu kuwa mtu mzuri wa kuibua stori. Kwa kifupi, nimejitokeza kama mwanaume wa kuvutia.

Upo!? [Soma: Sanaa za Kutongoza za Nesi Mapenzi]

Psss! Nakushauri uingie katika group letu changa la Facebook kwa jina Nesi Mapenzi ambapo utanipata huko nikijibu maswali ambayo uko nayo, plus utapata nafasi ya kutangamana na wote ambao husoma maujanja ya blog hii ya mapenzi.

Kwa Nini Wanawake Huwakataa Wanaume Flani

Ushawahi kujiuliza kwa nini wanawake wengine ukianza kuwatongoza wanakupa jibu zito ambalo unashindwa kulielewa la: "Mimi na wewe ni kama marafiki"?

Jibu hili hupokewa na wamaume wengi ambao bado hawajakomaa katika nyanja ya kutongoza na kudeti wanawake.

Hili ni tatizo ambalo mara kwa mara hujitokeza iwapo hautaufuata mpangilio stahili ambao unapaswa kuutumia unapoaproach mwanamke.

Unajiona ya kuwa unatongoza mwanamke, kila kitu unachofanya ama unachotaka kutoka kwake anaitikia (isipokuwa muingiliano kimwili), lakini ile siku unapoamua kuufungua moyo wako na kumwambia ya kuwa unampenda anakuzima na kukatiza matumaini yako ambayo ulikuwa tayari umeyaweka katika akili yako.


kwa nini wanawake huwakataa wanaume

Kutaka kujua kwa undani swala hili (tayari sababu zake tulikuwa twazijua) tuliamua kukusanya maoni kutoka kwa baadhi ya wanawake warembo kutaka kujua ni kwa nini wanawakataa wanaume ambao wamekuwa wakijaribu kuonyesha upendo wao kwa muda mrefu. Na majibu tuliyoyapata yalikuwa mamoja, yaani walikuwa wakilenga swala moja kuu ambalo lilikuwa likiwachosha.

Nalo ni...

Wanaume ambao hujionyesha kuwa ni watulivu na wasiokuwa na pupa.

Ok mbona wanaume aina hii wanawachosha wanawake na mwishowe kuwakataa?

Kulingana na maoni ya wanawake hawa ni kuwa wanaume aina hii huonyesha tabia ambayo inawafanya automatically kuwaingizwa katika kategoria ya 'marafiki'

Hivyo kutoonyesha matamanio yako kama mwanaume kwa mwanamke ama kuonyesha kuwa wewe ni mwanaume mnyenyekevu kunakuchongea wewe katika azma yako ya kumshawishi mwanamke yeyote.

So makosa ya mwanaume aina hii ni yapi?

Ok hebu tuichukulie mifano ifuatayo...

Je wewe ushawahi kuaproach mwanamke na kumwomba namba yake ya simu kwa kumwambia: "Hello, unaweza kuniazima namba yako ya simu? Labda siku moja tunaweza kuwa pamoja..."

Ama unapomuagiza kutoka naye deti unamwambia: "Hi, kikundi changu kinakutana siku ya Jumamosi, naonelea uungane nasi, itakuwa siku ya furaha..."

So tatizo hapa linajitokeza kivipi?

Wanawake wanapenda mwanaume mwenye nishati, nguvu na uwezo wa kuamua haraka haraka, mwanzo akiona mwanaume aina hii huwa anasisimka papo hapo. Unamuacha na maswali ya kutaka kujua zaidi kuhusu maisha yako ya undani.

So kuonyesha nishati aina hii utafanyaje?

Wakati mwingine ambapo utakutana na mwanamke unamwomba namba yake, toa simu yako, mpatie na umwambie hivi: "Shika. Niwekee namba yako kwa simu yangu. Ntapenda nikutoe out siku moja." [Soma: Mbinu tofauti tofauti za kumwomba namba mwanamke zenye uzito]

Kufanya jambo hili moja pekee kutakuwa kumekufanya ujitokeze kama mwanaume mwenye kujiamini, mwenye nguvu, na nishati ambaye anapigiwa upato na wanawake wengi. Na kamwe hatakuweka katika kategoria ya 'friend zone'

Ni rahisi ama?

Ok wakati mwingine unapoaproach mwanamke nataka uonyeshe nishati yako kama mwanaume, nataka uonyeshe kuwa wewe si mwanaume wa kuingizwa katika kategoria ya 'urafiki'. Mwanzo nataka uonyeshe ushupavu wako kwa kuzitumia mbinu tatu ambazo zitamfanya mwanamke akuheshimu sehemu yeyote pale ambapo atakuona. Nataka udhihirishe ya kuwa wewe ni mwanaume alpha ambaye hatikishiki na jambo lolote lile.

Jinsi Ya Kuwasiliana Na Wanawake Na Mbinu Ya 'Wapatanishi Mateka'

Ok najua ushawahi kuona jambo kama hili katika sinema si mara moja wala mara mbili...

Majambazi waliobanywa ambao wamevamia benki wakiwa ndani na bunduki zao huku wakitishia kuua mateka wao...

Ama jamaa ambaye amekumbwa na misongo ya mawazo (stress) amesimama katika ncha ya ukuta wa jumba lenye ghorofa 30 na anatishia kujirusha...

Hatua aina hii utapata polisi wakimuita mtu mahususi aka mpatanishi ambaye atahitajika kuongea na watu aina hii kwa amani bila kutokea jambo lolote baya...

Watu hawa huwa wamefundishwa spesheli kutatua aina hii ya migogoro na hakuna anayeweza kuwashinda kwa ujuzi wao dunia hii. Wanajua jinsi ya kutumia maneno na lugha MAHUSUSI ambayo itamfanya mtu kusisimka kihisia na kuweza kuwakontrol vile ambavyo wanataka wao.

Wanayajua maneno ambayo yanafanya kazi kama hirizi ambayo yatamfanya mtu kutulia na kumfanya aamini kila kitu ambacho ataongea.

So, je mbinu hii unaweza kuitumia kwa mwanamke?

Mbinu hii mwanzo ni rahisi sana kuitumia kwa mwanamke. Hii ni kwa sababu mara ya kwanza unapokutana na mwanamke na kuanza kumuongelesha huwa hajiskii huru na uwepo wako, huwa kwa kawaida anajiskia kama wewe uko hapo na unamtatiza shughli yake ambayo alikuwa akifanya. So kitu cha kwanza cha kufanya huwa unajaribu kumuonyesha kuwa wewe ni mtu salama na unaomba muda wake kiasi uongee naye (inajirudia katika hali ya mtekaji nyara na mpatanishi)

Zama nami...

Ok mwanzo nafaa nianze kwa kueleza hivi kwa wale ambao hawajajua mbinu hii.

Kuna kitu ambacho huwa kinatokea katika situation ya utekaji nyara: Watekaji nyara kwa kawaida huwa na hofu mwingi muda wote. Kwa kawaida hukumbwa na misongo ya mawazo muda wote ambao watakuwa na mateka wao.

Hii ni kama vile mwanamke anapopandwa na misongo ya mawazo asiyoweza kuizuia wakati wowote ambao mwanaume asiyemjua anamuapproach na kuanza kumtongoza.

So katika hali kama hii, unapaswa kujua jinsi ya KUONDOA misongo yake ya mawazo na UJENGE MSHIKAMANO na yeye haraka iwezekanavyo.



Unapaswa kutumia maneno yafaayo ambayo yatamfanya apumzike na kutulia...

Na kufanikisha haya yote hupaswi kutumia maneno ambayo yanachosha kama vile...

"Hivi wewe waitwa nani?"
"Ushawahi kuwa hapa awali?"
"Unafanya kazi gani?"

....na maneno mengine aina hii ambayo yanachosha.

Hapa lazima utumie maneno ambayo yatakuwa kama kitufe ambacho ukikifinya tu atakufungukia na kukuambia kila kitu ambacho unataka aseme...

Na unayavuta maongezi yenu mbali na 'sehemu hatari' ambazo zinaweza kusababisha yeye kupoteza hamu na wewe (90% ya wanaume hufanya MAKOSA HAYA ya kuleta mada ambazo zinawaudhi wanawake...)

Na wakati uo huo, unaingiza mbinu na maujanja rahisi ambayo yatachangamsha hisia chanya na kuondoa ukinzani wowote...

Kwa lugha nyepesi namaanisha ya kuwa lazima ujue jinsi ya kucontrol

Zifuatazo ni baadhi ya hali na jinsi ya kuzitatua...

Hali: Unataka kumtoa out mwanamke lakini hujui ni vipi atareact.

Mbinu: Watekaji nyara huwa wanapenda kuhakikishiwa usalama wao iwapo watajisalimisha kwa amani. Hivyo mpatanishi huelezea kabisa yale yote ambayo yatakayojiri baada ya kujisalimisa ili kuondoa woga wowote.

Atasema hivi: Nataka tu ujue Papito, kama utajitokeza na kuongea na mimi, hakuna mtu atakutatiza. Ni mimi na wewe tu ambao tutaongea...hakuna cha zaidi.

Vivyo hivyo kwa mwanamke, unafaa kumwambia yatakayojiri. Bila hivyo atakuwa akijiuliza ni KITU GANI ambacho kitakachotokea akikubali mwitikio wako wa kutoka out na wewe.

(Je unajaribu kuingia katika chupi yake? Ama wataka kumpeleka katika sehemu ambayo itamboa na ambayo haitamstarehesha? Ni kitu gani ambacho kitatokea kati yako na yeye??)

Mwambie hivi: "Nataka kukupeleka katika huu mkahawa/klabu ambayo niliivumbua hivi karibuni... ni sehemu nzuri ambayo naamini utaipenda kwa sababu wanacheza nyimbo nzuri na za kuvutia, mwanzo sehemu hii inalingana na ladha yako. Ntakuwa huko usiku wa Ijumaa, mbona tusiende pamoja na wewe wakati wa saa tatu usiku? Huwa sipendi kuchelewa sana nikiwa nje usiku lakini nikiwa na wewe nitaspend muda mrefu kiasi na wewe ili tujiinjoy zaidi...."

Hapa utakuwa ushaeleza matokeo yote yatakayojiri akiwa na wewe usiku huo.

(Kwa kutumia mbinu hii, utakuwa ushamjulisha matokeo yote ambayo yatatokea USIKU HUO kimukhtasari, lakini utakuwa umeweka plan yako kwa njia ambayo inaonekana ni nzuri na ambayo haimtishii. Utakuwa umerahisisha kwake kukubali na kusema "ndio")

******

Hali: Anaendelea kuzidi kukutajia kuhusu ex boyfriend wake, na kila wakati akimtaja anaharibu hisia za mazungumzo.

Mbinu: Mfanye ex boyfriend wake asionekane na thamani yeyote na 'kuziondoa nguvu zake zote' kwa  kumrejelea kama "yule mwanaume"...halafu unajeuza mada mliokuwa mkiongea.

Mfano...

Wewe: "Unajua Mamito, inaonekana kama YULE MWANAUME kiukweli hakuwa katika level yako hivyo ilikuwa jambo zuri kuachana naye. Nahisi kuna mengine muhimu zaidi ambayo yanakufaa kumliko...hebu niambie zaidi kuhusu kazi yako, naona inavutia zaidi kuona kuwa wewe ni (TAJA KAZI ANAYOFANYA)"

Wapatanishi hutumia mbinu ii hii wakati wanapotaja 'bunduki' ama 'bomu'...hakuna wakati watasema "Nataka uishushe bunduki yako," hii ni kwa sababu hilo NENO MOJA litamsisimua mtekaji nyara na kuongeza levels zake za stress.

Badala yake, wao husema "Ni mimi na wewe pekee tunaoongea, Papito, so nataka utulie na uweke HICHO KITU chini..."

(Na kufanya hivi wanaanza kuongea kuhusu maswala mengine ambayo yanajenga mshikamano wa nguvu...)

Psss...soma (sehemu ya pili ya chapisho hili)

Sababu 5 Za Kutongoza Wanawake Ufuoni Mwa Bahari

k. Inaweza kuonekana jambo la kufurahisha, lakini katika Nesi Mapenzi, tunaona ya kuwa ufuoni mwa bahari ni sehemu moja nzuri zaidi ya kukutana na wanawake wapya. Kama unaishi karibu na ufuo wa bahari halafu hujajishughulisha kutafuta mchumba huko basi ni wakati wako wa kufikiria mara ya pili: Tumia muda wako vizuri kwa kumakinika na kuapproach wanawake sehemu hizo na utakuja kugundua kwa nini tunasema kuwa beach ni sehemu moja muhimu ya kuapproach wanawake.



Na kwa kusistiza msimamo wetu, tumekuja na sababu zifuatazo:

1. Kunafurahisha
Hakuna njia mbili kuhusiana na swala hili: Ufuo wa bahari huwa ni sehemu inayofurahisha. So wakati ambapo unaanza kuongea na mwanamke katika ufuo wa bahari, nafasi kuu zaidi ni kuwa tayari anaenjoy muda wake katika sehemu hio. Hii inamaanisha hakutakuwa na haja za kuziondoa hisia zozote hasi. Atakuwa anafuraha, mcheshi, anajienjoy, na pia itakuwa rahisi kwake kukusikiliza kwa urahisi kwa sababu muda wote amejawa na furaha. Katika ufuo wa bahari ni rahisi sana ukilinganisha na maktabani, gym ama hata katika mkahawa. So tumia hii nafasi inayojitokeza.

2. Unakuwa mchangamfu
Ok. mtakubaliana nami ya kuwa hakuna mtu atajipeleka kwa ufuo wa bahari kama hana kitu cha kufanya. Kwa kawaida mtu akienda beach huwa lengo lake kuu ni kuogelea, hujumuika na marafiki zake, kucheza mpira, kukimbia ama jambo lolote lile ilimradi tu aonekane yuko mchangamfu na shughli flani. Kumhusisha mwanamke katika shughli zako ni njia muhimu na ya kwanza kuchukua ili uweze kumfahamu zaidi. Bora zaidi ni kama unafanya beach party, unaweza kumualika kwa marafiki zako. Cha zaidi ni kuwa wakati ambapo unaonekana mchangamfu, pia unaonekana bora, jambo ambalo ni muhimu.

3. Ni sehemu ambayo wanawake hupenda
Kila mtu anajua ya kuwa sehemu za ufuo wa bahari kuna wanawake wengi zaidi kuliko sehemu zozote zile ambazo zinajulikana. Kama unataka kukutana na wanawake basi ni lazima uende katika zile sehemu ambazo wanapatikana. So bila kupoteza wakati wako unafaa utembelee sehemu hizi haswa beach ambayo uko karibu nayo uweze kutangamana na wanawake tofauti tofauti.

Halafu alama muhimu hapa ni kuwa katika beach kwa kawaida wanawake huwa wamevalia bikini na vinguo vya kuogelea. So kama unatafuta sehemu ya kutafuta wanawake, hata si jambo la kutumia ubongo. Hivyo basi mbona hujaenda kwa beach tayari?

4. Hisia zako zinakuwa juu
Uko mchangamfu, unaangazwa na jua la ufuoni na unajienjoy. Kuna nafasi gani nyingine unangojea upewe ili uongee na wanawake? Sehemu kama hii unapaswa uonyeshe hisia za juu, ujihisi bingwa na kufurahia wakati unapoongea na wanawake. Kama wewe ni mwanaume ambaye unapenda beach halafu unapenda maji, hakuna njia mbili za kuchagua, lazima uende baharini na uanze kukutana na wanawake wapya, sehemu ambayo itainua hisia zako.


5. Ni romantic
Labda maswala ya romantiki huna lakini yeye akawa nayo. Huu hapa ni uzuri wa romantic ambazo zinajikuza kutokana na mapenzi ya baharini: ni kuwa neno 'Nimefurahi kukutana na wewe" litajeuka kuwa "nataka kukujua zaidi" hadi likawa "nakumbuka ule wakati tulipokutana mara ya kwanza...".

Hakuna sehemu nyingine yeyote ile ambayo unaweza kuwa na nafasi ya kuupiga jeki uhusiano wako na mwanamke ambaye umekutana naye kidharura isipokuwa katika ufuo wa bahari. [Soma: Siri za kumvutia mwanamke]

Kwa Nini Hupaswi Kutongoza Kwa Mtandao Wa Facebook

Kulingana na takwimu  ni kuwa mtandao wa Facebook una watumiaji zaidi ya bilioni moja. Hii ni kama asilimia 14 ya watu ulimwengu mzima. Takwimu hizi zinamaanisha ya kuwa katika mtandao wa Facebook kuna wanawake wengi sana ambao unaweza kuamka asubuhi na kuanza kutongoza mchana na usiku mzima.
Mwanzo Facebook inarahisishia kazi yako kwa kuwa inakuletea majina ya wanawake warembo ukiulizwa kama unataka kuunganishwa na wao.

Lakini swali ni je, mtandao wa Facebook kweli unafaa kutumiwa kutongoza wanawake?



Kama uliingiwa na tamaa ya kutongoza mwanamke katika mtandao wa Facebook tunakuambia uachane na mpango huo haraka iwezekanavyo. Kuna mitandao mengine ambayo imewekwa hususan ya kutongozana.

Hizi hapa ni sababu za wewe kuacha na kutongoza wanawake katika mtandao wa Facebook.

1. Ni bora zaidi kutongoza kwa kuonana
Kutongoza kwa Facebook si njia murua ya kutongoza. Huwezi kutumia mbinu za kupapasa, miondoko ya mwili, uso na hata toni ya sauti yako - mambo ambayo ni muhimu sana ikija na maswala ya kuvutia wanawake. Bila kutumia mbinu hizi mwanamke anaweza kutoelewa ujumbe wako vile unapaswa kuupitisha. Mbinu za mapenzi fioa ama vichocheo vyako vya mapenzi ulivyotumia vinaweza visitambulike. Ama kuonekana kuwa na nia mbaya ama kuonekana na ajenda mbaya.

So badala ya kutegemea Facebook, tongoza wanawake moja kwa moja. Kama hujui ni vipi vya kuanza wewe anza kumshika mwanamke kwa kumpapasa wakati mnapokuwa mkiongea. Anza kwa miguso mepesi kwa kiko chake. Ukiona anaingiliana unaweza kuongeza miguso yako kwa sehemu zake binafsi zaidi. [Soma: Jinsi ya kutongoza kama bingwa]

2. Kupungukiwa na uwezo wa kutongoza kiuso
Sababu moja ambayo hupaswi kutongoza wanawake katika mtandao wa Facebook ni kuwa utapungukiwa na uwezo wa kutongoza mwanamke uso kwa uso. Kama unajijua ya kuwa wakati wote unachat na mwanamke kupitia mtandao wa Facebook basi unaweza kujihisi hutohitaji kumtongoza wakati ambapo mtakuwa pamoja. Haya yatakuwa makosa makubwa, kwa sababu kama tulivyoelezea awali ni kuwa kutongoza uso kwa uso ni muhimu zaidi kuliko kutongoza online.

Kuhakikisha ya kuwa haukosi nafasi yeyote ya kutongoza wanawake ambao wamekuvutia, anza kwa kufuata sheria ya kuapproach wanawake. Wakati ambapo umekutana na mwanamke ambaye unataka kuongea naye ama kumtongoza, mfuate na uanze kuongea naye dakika mbili za kumuona. Usifikirie, wewe mfuate. Jifunze tabia ya kuchukua hatua za haraka kwa mwanamke na utaona ukifanikiwa kwa haraka kuliko kutegemea mtandao wa Facebook. [Soma: Toa uoga wa kuapproach mwanamke]

3. Ujumbe wako unasahaulika mapema
Facebook inaweza kuwa sehemu ngumu ya kujieleza. Kuna jumbe nyingi na mpya ambazo zinahitajika kusomwa, habari za kubofya, na mambo mengine yasiyokuwa na maana ambayo yanaweza kufanya ujumbe wako kupotea katika mazingira haya. Mambo haya yote lengo lake kuu ni kuchukua attention ya mwanamke, kumaanisha ya kuwa itakuwa vigumu zaidi kwa wewe kuweza kujieleza ama kuiteka attention ya mwanamke.

Kama unataka kutongoza mwanamke kwa mtandao, sehemu nzuri zaidi ni kwa mitandao ya kudeti. Huko utapata wanawake ambao wako active wakitafuta kufurahishwa, kupendwa na kutongozwa. Washindani wako hapa watakuwa wanaume pekee - ambao asilimia 90 ya hao wanatuma jumbe za kuboesha aina moja. Kama utasimama na kutuma ujumbe mfupi,  wakuvutia na wenye msisimko wa kimapenzi (sana meseji ambazo zinaonyesha ya kuwa unasoma profile yake) - utakuwa na upeo mpana wa kuweza kuwa na mafanikio ya kutongoza wanawake kwa mitandao ya kijamii.[Soma: Orodha ya mitandao spesheli ya kutongoza]

4. Inaendelea kuzeeka
Ni sawa kusuka wanawake mara moja au nyingine katika Facebook, kama tu lengo lako ni kujinoa makali, lakini itafikia wakati flani utaingiwa na hamu ya kuvuka katika level nyingine. Utahitaji kuchukua namba yake ya simu, ama zaidi kukutana naye. La sivyo  maongezi yako yataanza kuoneka kuzeeka na kukwama kuendelea zaidi.

Wakati mzuri wa kuomba namba yake ni wakati ambao maongezi yenu yanaendelea vizuri - wakati ambapo anajibu meseji zako kwa uharaka. Na jinsi ya kumuomba namba kutalingana na jinsi utakavyomuomba, hapa lazima uonyeshe nia na ulenge moja kwa moja. Mpatie wakati mahususi na sehemu ambayo mtaamua kukutana.

5. Inakupa chapa mbaya
Kutuma meseji nyingi kwa Facebook kunaweza kuwapatia wanawake taswira ya kuwa hauna kitu cha kufanya ila unapoteza muda wako mwingi kwa Facebook. Ok, hio si dhana ambayo unataka kuipitisha kwa mwanamke yeyote. Unataka kumuonyesha ya kuwa wewe una mambo muhimu zaidi ya kufanya katika maisha yako. Unataka kumuonyesha ya kuwa una maisha ambayo unatamani yeye awe nayo.

Njia rahisi ya kuonyesha wanawake katika mtandao wa Facebook ya kuwa una maisha yako ni kuonyesha kuwa maisha yako ni ya furaha. Jipe shughli kwa kufanya shughli zako, tangamana na wengine na kujumuika katika matukio tofauti tofauti. Kufanya hivi kutapandisha hadhi yako na itakuwa rahisi kwa yeye kuweza kupendezwa nawe. [Soma: Jinsi ya kumuonyesha mwanamke una maisha yako]
6. Ni sehemu mbaya ya kutafuta wachumba
Kuna baadhi ya wanaume ambao wanadhani ya kuwa mtandao wa Facebook ni sehemu nzuri ya kupata wanawake wapya. Watajaribu kuwafikia wanawake wapya ama marafiki wa marafiki zao ambao wanafikiria ni warembo na kuanza kuwatongoza. Tatizo ni kuwa wanaume aina hii huharibiwa ama kupewa picha mbaya kuwahusu na marafiki zao, na wanapoteza muda wao mwingi ambao hautawapeleka mahali popote kwa hao wanawake.
Njia bora zaidi ya kukutana na wanawake kupitia kwa marafiki zako ni kuwaalika marafiki zako katika party ama kesha mjini. Unaweza kuambia kila rafiki yako aalike rafiki yake ili ajiunge kwa kikundi, kama njia ya kupanua jamii yako ya kutangamana. Njia hii unaweza kujuana wanawake wapya na warembo zaidi ukilinganishwa na kutuma meseji za kubahatisha kwa wanawake usiowajua katika mtandao wa Facebook.[Soma: Zijua sehemu za kukutana na wanawake]

Jinsi Ya Kuwa 'Classy Man' Utongoze Wanawake

Kwa muda nimekuwa nikiushabikia huu wimbo wa Jidenna wa 'Classic Man' kwa kuwa unavutia kwa sauti na maneno ambayo yanatamkwa katika nyimbo hio. Cha kushangaza ni kuwa wimbo huu umependwa sana na wanaume kuliko wanawake. Ok, kwa kuupitia wimbo hii kijuu juu ni kuwa Jidenna anajaribu kujieleza ya kuwa yeye ni mwanaume 'classy', yani mwanaume ambaye ana taasubi za watu wa zamani kimaisha, wanaume wale ambao waliyatambua na kuyaenzi maisha yao kiusafi, kifasheni, kuwa na taasubi za kiume nk.



So kwa kutumia kigezo cha kuwa 'classy', hapa Nesi Mapenzi tumeamua kuandika chapisho spesheli kuhusiana na kigezo cha mwanaume 'classy' kwa kuwa imeonekana kuwa tabia ya mwanaume aina hii inaenziwa mpaka karne ya sasa.

So unataka kuwavutia wanawake?

Kuna wanaume wengine mpaka sasa hawajasahau wala kutupa tabia hii ya kuwa 'classy'. Mwanzo wanawake huvutiwa automatic na wanaume ambao wana tabia aina hii katika maisha yao. Lakini pia kuwa 'classy' pekee hakutakusaidia kuweza kuvuta na kunasa mwanamke yeyote, lazima uwe na ujiaminifu wa kiwango cha juu. (Machapisho yetu ya awali yanafafanua zaidi).

Hizi hapa ni hatua ambazo zitakusaidia kuwa na tabia za uclassy.

1. Usingojee uthibitisho kutoka kwa wengine
James Bond ni mfano mzuri tunaoweza kuufikiria wa mwanaume ambaye ni classy. Ni jambo gani linalomfanya kuwa hivyo? Hangojei wala kutaka uthibitisho kutoka kwa wengine. Mvuto-ushawishi wake si kuwa anavalia tuxedo za kuzuzua, bali ni kwa sababu ni mwanaume ambaye hahitaji kuambiwa na yeyote yule kuwa yuko SAWA - tayari anajua. Kama kuna watu ambao watakubali na kujiunga naye, ni vizuri. Kama hawataki, hakuna tatizo pia. [Soma: Mbinu ya kufanya ili uweze kujiamini]

2. Valia ipasavyo
Kuna watu wanajidanganya ya kwamba kuwa mwanaume classy lazima uwe umevalia suti ya three piece kila mahali ambapo utaenda. Ok ukweli ni huu...kuwa classy kunaangaliwa zaidi na vile unavalia nguo zinazokufaa zaidi kuliko kuvalia nguo ambazo zitakuanika kama mwana fasheni. Classy ni kuvalia nguo ambazo zina hadhi ya juu kuwaliko wengine lakini pia unavalia kulingana na hulka yako.

Mwisho wa siku ni kuwa wewe mwenyewe ndio utajifahamu iwapo ni wewe halisia ama ni mwigo. Kama unashindwa na kutafuta nguo ambazo zitakuweka classy unaweza kuenda katika duka la nguo karibu na wewe ukajigeze. [Soma: Jinsi ya kubadisha mwonekano wako uvutie]

3. Gonga ndipo
Kwa blog tumekuwa tukiligusia hili swala kwa kina na mfano mzuri tukauweka kwa Leonardo Di Caprio. Jambo ambalo yeye hufanya kwa  kuwasiliana kiujiaminifu na uvuto ni kuwa anaongea moja kwa moja. Hii kwa kawaida ni kuonyesha tabia ya uclassy, kwa sababu unaonyesha uadilifu kwa kitu ambacho unaazimia kutaka ama kufuatilia. Hakuna makosa yeyote kusimama na kumuapproach mwanamke katika klabu ama baa na kumwambia "Nimekuona ukisimama katika ile sehemu na nimetaka kuongea na wewe." Maneno haya najua hayafai kuishia hapa, lakini umemwendea direct na kugonga ndipo kuhusu ajenda yako, jambo ambalo huonekana kuwa classy. [Soma: Jinsi ya kugonga ndipo kama Leonardo]

4. Chukua namba yake kama mwanaume classy
Jambo ambalo linakuwa changamoto kwa wanaume wengi hadi sasa ni kuona wakitatizika kupata namba kutoka kwa mwanamke. Hapa tumekuandikia mbinu ya kuomba namba kiclassy (tofauti na mbinu tulizozipendekeza awali)

i) Mwombe namba yake wakati ambapo maongezi yenu yamefikia kileleni, si ule wakati ambapo uko karibu kumaliza maongezi.

ii) Usiweke lionekane kama swali. Badala yake, unamwambia kuwa unataka namba yake ili uweze kukutana na kuongea naye wakati mwingine.

iii) Weka simu yako tayari kupokea namba yake ya simu.

iv) Mpatie simu yako kwa kuiweka sehemu yake anayoichukulia binafsi.

v) Wakati anapoandika namba yake kwa simu yako, gusia kuhusu maswala ya deti ukilenga gumzo ambalo mumekuwa mkiongea awali.

vi) Mtumie jumbe papo hapo wakati amekurudishia simu yako ili aweze kupata namba yako. Mtumie jumbe nyepesi na ya ucheshi. Mfano "Ni P.p.T, yule mwanaume mwenye tabasamu la kuua. :-D" [Soma: Mbinu ya kumfanya mwanamke alazimike kukupatia namba yake ya simu mwenyewe]

Jinsi Ya Kumsisimua Mwanamke Kabla Ya Kulala Naye

Wakati umemualika mwanamke sehemu unayoishi ama wakati umetoka deti katika bar, unapaswa kujua ya kuwa kumsisimua mwanamke huanza kabla ya nyinyi wawili kulala pamoja.



Unapaswa kumsisimua kuanzia nafasi ya kwanza ambayo utaipata kutoka kwake. Kufanya hivyo kutamfanya akutake hata zaidi na kumfanya ajiandae na mapema kabla hata kulala naye. Lakini ni mbinu gani inayoweza kutumika kumsisimua mwanamke kabla hamjalala pamoja?

Zama nami...

Kutumia maneno
Maneno yanaweza kumsisimua mwanamke asilimia mia. Mwanzo wanawake husisimuliwa na vitu wanavyosikia zaidi kuliko wanavyoona. Hii ndio tofauti kuu kati ya jinsi ya kumsisimua mwanaume na mwanamke. Hauhitaji kuonekana mchafu wakati ambapo unamsisimua mwanamke kwa kutumia maneno. Mwanzo anaweza kusisimulika na jinsi ambavyo anakusisimua wewe. Unaweza kumwambia maneno kama "Siwezi kungojea ile siku ambayo nitakuwa pekeangu na wewe", "Nimeanza kuingiwa na mawazo nikifikiria hio nguo uliyovaa inaficha nini" ama maneno mfanano na haya.

Lakini kando na kuwa maneno yanamsisimua mwanamke, kutategemea pia na vile ambavyo unamshika na miguso yako.

Kutumia miguso
Hapa ndipo utaleta utofauti wa yote. Miguso ni mbinu nzito na ya nguvu kama unaazimia kumfanya akutamani, kabla hata nguo za yeyote kuvuliwa, kabla ya nyinyi wawili kuanza kubusiana ama kufanya chochote. Baadhi ya mifano ya kufuata ya kumsisimua mwanamke kwa miguso ili aweze kukutamani kabla ya nyinyi wawili kulala pamoja ni kama ifuatayo: [Soma: Hatua za kumfanya mwanamke awe huru unapomgusa]

Kuzivuta nywele zake kiulaini: Usizivute nywele zake hadi ukazing'oa kichwani mwake. Lakini usiogope kuzishika baadhi ya nywele zake na kuzichezea kimvuto.

Miguso ya kukawia: Wakati ambapo unamgusa kikawaida - kwa mfano, wakati mikono yako iko katika mabega yake, mgongo au mkono - usiogope kuuzuia mkono wako ukawie sehemu hizo kwa dakika moja.

Karibu kumla dende: Hii ni siri kubwa ambayo inahakikisha gemu yako kuwa ya juu. Usikimbilie kumbusu. Jiweke katika hali ambayo nyinyi wawili mko "karibu" kubusiana. Hii itamfanya aingiwe na wazimu wa kutaka kuibusu midomo yako haraka kuliko ulivyokuwa ukitarajia.

Kumkwaruza kiulaini: Unapomgusa, usiogope kuzipitisha kucha zako kwa mgongo wake, nyuma ya shingo yake na sehemu mfanano na hizi. Hii unaweza kuitumia wakati ambapo mshajenga uhusiano wa ndani kati yenu.

Mtizamo wa macho: Kumuangalia mwanamke kwa macho pekee kunaweza kumfanya apandwe na mzuka. Mwangalie machoni, zaidi kuliko yeye. Kufanya hivyo kunaashiria ujiaminifu. Ijapokuwa mbinu hii haitumii miguso, inaweza kufanya kazi sawa na kama vile matumizi ya miguso kabla nyinyi wawili kulala pamoja.

Ok hizi ni baadhi ya mbinu za kumfanya mwanamke asisimke kabla kulala na yeye. Unaweza hata pia kuamua kumpandisha nyege bila kutumia miguso yeyote.

Sunday, April 29, 2018

Hatua Za Kuapproach Wanawake Katika Kikundi

Kuapproach wanawake wakiwa katika kikundi ni jambo gumu sana kwa mtu yeyote kutimiza. Hata kwa wale ambao wanajiamini mbele ya wanawake inafikia wakati flani wanapatwa na changamoto moja au nyingine. Lakini kama kawaida mambo kama haya yanaeleweka kwa kuwa unaaproach wanawake wengi wakati mmoja na pia kunaweza kutokea maswala mengine ambayo yanaweza kujeuka changamoto kwako.



Kuapproach wanawake wakiwa kwa kikundi si sawa na kubadilisha gemu ya kutongoza mwanamke mmoja bali ni mbinu tofauti kabisa ambayo inahitajika kutumika. Mbinu ambayo lazima uijue na kuielewa.

Kwa nini unahitajika kujua kutongoza wanawake katika kikundi

Jambo muhimu ambalo unapaswa kujua wakati unapoapproach wanawake kwa kikundi ni kuwa unaaproach kundi zima, na wala si mwanamke mmoja ambaye unataka kuongea naye. Kama unaaproach kwa kikundi, ni vyema uende pekeako. Mkiapproach kama kikundi mnaweza kuonekana kuogopesha na wanyemelevu, hivyo ni vizuri zaidi kama marafiki zako watangojea kwa dakika, ili uweze kuwatambulisha vyema kwa kikundi hicho cha wanawake.

Wasalimie wanawake wote wakati mmoja
Ikija na swala la kusalimia wanawake katika kikundi, ni vizuri kuwasalimia wote wakati mmoja. Vile ambayo utawasalimia wanawake katika kikundi ni kama vile utakavyomsalimia mwanamke mmoja; unatoa matamshi ya mizaha na ucheshi, halafu inafuatiliwa na tabasabu halafu sasa unaanza kufunguka zaidi kwa kuongea zaidi na wale wana kikundi ambao wanapenda kuongea. Ni bora kuwasalimia wanawake wote kwa wakati  mmoja hata kama kuna mwanamke kikundini ambaye ulitaka kumvizia ama kuongea naye. Hii haitaonyesha ya kuwa unakimbilia kukutana na mwanamke mrembo pekee, bali unajionyesha ya kuwa umekuja hapo kujumuika na watu na kuinjoy muda wako ipasavyo.[Soma: Mbinu asilia ya kumfanya mwanamke akupende]

Ipunguze makini yako
Pindi unapoendelea kuongea na wanawake wote, halafu rafiki au marafiki zako wakatokezea, inakubalika kupunguza umakini wako hadi kwa mwanamke mmoja au wawili. Labda bado unataka kuongea na mwanamke ambaye ulimpangia kuongea naye, ama umepata mwanamke mpya kutoka kwa kikundi hicho, unaweza kuyapendua maongezi yako zaidi. Unaweza kuanza na maneno rahisi kama "nimependezwa nawe" ama "unaonekana uko sawa." Hapa unapaswa kumsifu mwanamke kando na umbo lake, halafu baadaye uanzishe gumzo la "nataka kukujua zaidi"

Jaribu kuwa na kisaidizi
Kuwa na kisaidizi wakati unaaproach wanawake katika kundi kubwa inakuwa rahisi sana. Kwa mara, wanaweza kuchat na wanawake wale wengine huku wewe ukimakinika na mwanamke mmoja ambaye ulikuwa umeazimia kukutana naye. Zaidi ni kuwa wanaweza kutoa presha ambayo inakuja wakati unapotaka kuapproach, hii inasaidia kwa kuwa inakupa ujiaminifu kama mwanaume wakati unapoapproach wanawake katika kikundi.  Sababu ni kuwa unajua kuwa usaidizi hauko mbali na wewe na muda wowote wanaweza kutokezea ili kuondoa presha zozote ambazo zinaweza kujijenga.

Mtenge mmoja kutoka kwa kikundi
Kama kuna mwanamke ambaye umeonyesha interest kwake, jaribu kutafuta wakati muwe pekeenu. Hii haimaanishi ya kuwa ni lazima mujitenge katika sehemu moja ya hio klabu ama baa bali pia inaweza kumaanisha ya kuwa unaweza kuamua kutoka ziara hadi katika mkahaha ama sehemu nyingine ya kuvutia ambayo itawaruhusu nyinyi wawili kupata nafasi ya kuongea moja kwa moja ili mjuane vyema zaidi.[Soma: Mbinu ya kutumia ili umtoe deti mwanamke]

Jinsi Ya Kuondoa Vizuizi Vya Mguso

Njia moja rahisi ya kupandisha level yako ya kutangamana ni kwa kutumia miguso. Kutumia miguso ni njia ambayo wanaume wengi wanashindwa kuielewa. Unaweza kupata mwanaume ambaye anadai 'kujiamini' anaanza kumgusa mwanamke kiholela holela mpaka mwishowe akapigwa kofi ama kukataliwa. Halafu kuna wale wanaume waoga ambao wako sawa kutongoza lakini wanaogopa kuchukua hatua ya kuanza kutumia miguso kwa mwanamke.

Well, haya ni mambo ambayo yanajitokeza mara kwa mara na inakubalika kwa kuwa wanaume wengi mpaka sahizi hawajaielewa stadi ya kutumia miguso.



Lakini kama unataka kuyafanya maongezi yako na mwanamke kuwa ya fanaka basi tunasistiza kuondoa kizuizi cha miguso.

So mbona tunasistiza kutumia miguso ili kuondoa kizuizi kati yako na yeye?


Kuvunja kizuizi cha mguso ni kuwa kinachochea kuongezeka kwa hisia kati yako na mwanamke unayeongea naye. Wakati unapotumia miguso kuongea na mwanamke, kuna nishati inayojijenga ambayo inasaidia mwanamke kuungana na wewe, hivyo kurahisisha kwake kuweza kukusikiliza, kukupatia namba yake na hata kukubaliana na wewe kutoka deti. Mwisho ni kuwa kutumia miguso unatuma meseji fioa ya kumwambia mwanamke kuwa yuko huru kwa yeye kukugusa.

Kugusa kunakostahili
Wakati mwingine wanaume wanaogopa jinsi watakavyoonekana wakianza kumgusa mwanamke. Hapa Nesi Mapenzi tumekuja na hatua mbili kuu ambazo zitakurahisishia wewe kumgusa mwanamke kwa njia inayostahili, na ambayo ni rahisi kwa yeyote kuianzia.[Soma: Jinsi ya kumpandisha nyege mwanamke bila yeye kujijua]

Kwanza, ni kuhakikisha ya kuwa miguso yako itaonekana kama mchezo. Hii inaweza kuanzia kwa kumdara sehemu yake ya bega halafu unamsalimia kwa tabasamu akigundua kuwa ilikuwa ni wewe ukimgusa. Kiujumla, unataka kufanya kila kitu kionekane ucheshi na utulivu sababu hii ni hatua za kwanza za kutangamana. Hii inatumika wakati wa kumgusa na kuongea.

Pili, ni umguse sehemu zake ambazo ni 'salama'. Hizi sehemu zinajumlisha sehemu ya juu ya mgongo, mikono, mabega na viganja. Hizi sehemu tunaziita 'salama' kwa sababu, tofauti na sehemu nyingine, sehemu hizi hazina swala lolote na mapenzi.

Ukitoka out usiku, jaribu kuonyesha michezo kwa kumgusa mwanamke katika mabega wakati ambapo unaongea naye. Halafu angalia yale ambayo yatajiri.

Miguso inafanya nini?

Wakati unatumia miguso kuwasiliana na mwanamke, kuna mambo ambayo hutokea kutokana na jambo hilo. Haya hapo ni baadhi ya mambo yanayotokea iwapo unataka kuvunja kizuizi cha miguso: 

#1. Inaashiria furaha: Kumbuka, miguso yako inafaa iwe ya furaha na kuchangamua. Miguso ni njia ya nguvu ya kuwasiliana hivyo ukitumia maneno na miondoko yako ya mwili kutachangia kufanya utangamano wako na yeye kuwa wa hali ya juu. Ukitumia miguso yako vizuri kwa mwanamke, kuna homoni inayoitwa oxytocin ambayo itamfanya mwanamke ajiskie vizuri.[Soma: Jinsi ya kumuathiri mwanamke na penzi lako]

#2. Unamfanya ajiskie burahi na miguso yako:  Wakati ambapo utamakinika kumgusa mwanamke, itafikia wakati flani atakuwa akijiskia huru na miguso yako, yaani hataona wasiwasi wowote wa kuona mikono yako ikilisha katika ngozi yake. Ukiona kuwa anakuachia nafasi ya kumgusa, unaweza kuongeza sehemu zako za mguso hadi zile ambazo anaziona ni faragha yake.

#3. Unampa ruhusa ya yeye kukugusa: Wakati mwingine inatokea kuwa mwanamke anahitaji umguse sehemu moja tu ili aweze kukupandilia. Kumgusa unatuma ujumbe wa kuwa ni SAWA kwa nyinyi wawili kugusana hivyo utakuwa umeupitisha ujumbe wako. Hivyo basi wakati ambapo umeongea na mwanamke kwa muda mrefu, unaweza kupitisha mkono wako hadi kwake halafu uangalie majibu kutoka kwake.

#4. Inavunja kizuizi: Miguso inakuwa kama daraja la kuondoa pengo lolote kati yako na mwanamke unayeongea naye. Kuunganika kimguso kunasaidia kujenga hisia kati yako na yeye. Kando na huwa atajiskia huru kukugusa, pia atajiskia huru kuongea na wewe. [Soma: Mbinu ya kumsisimua mwanamke na maongezi yako]

Mwisho ni kuwa usiwe na uoga wa kupeleka mkono wako kwa mwanamke. Ukiona una tatizika na jinsi ya kumgusa, unaweza kutafuta kisababu ambacho kitakufanya wewe kumgusa. Mfano unaweza kumuuliza "Unapaka mafuta gani? Mbona ngozi yako ni nyororo hivi. Naweza kuishika? ama unaweza kutumia tabia ya uclassy na kumwambia "Tangu nianze kuongea na wewe vidole vyangu vimekuwa vikiniwasha, na tiba yake itatotaka na kuigusa HII ngozi yako nyororo"

Jinsi Ya Kuwavutia Wanawake Bila Kutamka Neno

Ushawahi kujikuta katika hali ambayo unashindwa kujua utaanza vipi kuongea na mwanamke? Ni mwanamke mzuri ambaye moyo wako unamtamani lakini akili yako inashindwa kutengeneza mawazo ya jinsi utakavyoanzisha stori na yeye. Unabakiwa ukimuangalia akikupita mbele yako, ama mbaya zaidi anakuja kuchukuliwa na wanaume wasiokuwa na thamani yeyote kwa maisha yake. Unabakia na majutio na mawazo ya "kama ningeweza kujiamini mbeleni si ningem...." Well, tatizo hilo halijawahi kutokea kwako pekee bali kwa kila mwanaume wakati flani katika maisha yake na hatutaki lijitokeze tena mbeleni.



So chanzo cha wewe kutoweza kumtongoza huyu mwanamke ni kuwa akili yako ilikataa kutoa mazungumzo ambayo ungeweza kuyatumia kwa huyo mwanamke. Well, waonaje kwa mara moja tukubaliane na akili yako na tusitumie maongezi kuapproach mwanamke, na badala yake tutongoze kimya kimya?

Kutongoza kimya kimya ni mbinu rahisi sana, mwanzo ni rahisi kwa kuwa unapata kujua kama mwanamke anakupenda au la. So bila kupoteza wakati, hebu tuchambue mpango mzima.

Zama nami!

1. Kwa kutumia macho
Kila mtu anajua nishati inayotokana na kutumia macho. Macho ni kiungo ambacho wanaume wamebarikiwa nacho na akikitumia vizuri kinajeuka kama silaha nzito wakati ambapo unaitumia kwa mwanamke. Ushawahi kujiuliza ni kwa nini wakati mwingine mwanamke anashikwa na aibu/haya wakati unapomwangalia? Ama je ushawahi kumskia mwanamke akisema kuwa usimwangalie machoni mwake? Hii ni kwa sababu macho yanaweza kutumika kuongea maneno ambayo mdomo unaweza kushindwa kuongea.


Wakati utajipata ukimwangalia mwanamke, mwangalie machoni halafu utoe tabasamu. Kumuangalia kunaonyesha unajiamini. Kutabasamu unamwonyesha kuwa wewe ni salama na anaweza kuongea na wewe. Unaweza kusoma chapisho letu la awali ambalo linafafanua mbinu ya kutumia macho kuapproach mwanamke kwa kina.

2. Mfanye akugundue kupitia kutangamana kwako
Njia nzuri ya kusimama ili wanawake waweze kukutambua ni kupitia utangamano wako na wengine. Kujizunguka na wanawake wengi (haswa wale warembo) kutaashiria ya kuwa wewe ni aina ya mwanaume ambaye wanawake wanapenda kuwa naye. Hii itawafanya wanawake wengine katika hio sehemu kuwa na shauku ya kutaka kujua ni kitu gani ambacho kinakufanya wanawake wapende kuwa na wewe. Hii automatically itawafanya wanawake kuwa na umbea kukuhusu, kuvutiwa kwako, na hata kuingiwa na wivu wa kwa nini haujawaingiza katika kundi lako. 
Mbinu hii ni moja wapo ya sosholojia ya wanawake, kimaumbile wanawake hupenda vitu ambavyo wanawake wengine hupenda. Hivyo kama wewe unamtaka mwanamke flani na hutaki kutumia maongezi, anza kutangamana na marafiki wake wote isipokuwa yeye, mwishowe utamwona akijileta yeye mwenyewe, tena ujitayarishe na mapema kwa kuwa atakuja na presha ambayo kama hukujipanga vizuri inaweza ikakulemea.
3. Matumizi ya banta bila kuongea
Banta ni mbinu ya kuonyesha ucheshi, mchezo na mzaha wakati wa kuongea na mtu. Mbinu hii pia inaweza kutimizwa bila kutumia mazungumzo ili umfanye mwanamke aweze kuvutiwa kwako.
Kwa mfano, kama ulishatumia mbinu ya macho kuwasiliana na mwanamke na unataka kuendeleza shughli kwa kutumia banta, njia rahisi ni kumuonyesha nyuso za ucheshi. Jifurahishe na uwe mcheshi - toa ulimi wako nje - pinda macho yako - weka uso wowote ule wa kipuzi ambao unajiskia. Hii ni njia rahisi ya kumfanya mwanamke atabasamu akiwa mbali, na itakuwa rahisi kwako kumuapproach na kuendea na yeye iwapo ataonyesha dalili za kupendezwa na wewe.
4. Mvutie na mwonekano wako
Ukitaka kumvutia mwanamke kiurahisi basi ni muhimu kubadilisha mwonekano wako. Mbinu hii tuliieleza kwa kina katika chapisho la jinsi ya kubadilisha mwonekano wako uwavutie wanawake. Kwa kawaida, wanawake wanapenda kushufu wanaume ambao wanavalia kinadhifu.
Lakini hapa usichukulie makosa. Kubadilisha mwonekano hakumaanishi ya kuwa unapaswa kuvalia nguo ghali ama za thamani ya juu. La hasha. Kubadilisha mwonekano kunamaanisha kuvalia nguo safi, nadhifu na ambazo zinaashiria hulka yako. Usijitese kuvalia nguo ambazo haziwiani na wewe kwani kwa mwanamke ni rahisi kukugundua kama umejeuka mwigo.
5. Ishara ya mwili wako 
Wanawake wanaweza kujua mengi kukuhusu kwa kuangalia miondoko yako ya mwili pekee. Kama unataka kuonyesha ujiaminifu ambao utamfanya mwanamke akutambue, basi ni lazima mwili wako uonekana vile unapaswa kuonekana.
Kuonyesha confidence katika mwili wako unapaswa kufanya yafuatayo:
i) Simama wima - mwanaume thabiti akisimama anakuwa hivi; masikio yako yawe nyuma ya mabega yako, mabega yako yawe nyuma ya kiuno chako, kiuno chako kiwe nyuma ya kiwiko chako.
ii) Kaa kwa kujitanua - wakati umekaa katika kiti, hakikisha ya kuwa unachukua nafasi yote ambayo unaweza kuitimia. Egemea kwa kiti, itanue miguu na mikono yako, kichwa kiweke kiangalie juu.
iii) Jinsi unavyokaa - Usisogee sogee kama huna sababu zozote, usikunje miguu wala mikono, usiangalie chini, usijikune kichwa ama kutafuna tafuna.
iv) Unavyotembea - Tembea na sababu, tembea kwa kujiamini, tembea na njia thabiti.
Kuweza kukontrol mwili wako inakusaidia kuonekana mtu mwenye nguvu, wa kujiamini ambaye anapendwa na wanawake. [Soma: Jinsi ya kutumia mwili wako kutongoza]
6. Kuwa na hadhi ya juu
Mpaka sasa hili chapisho linaongea kuhusiana na kuwasiliana na mwanamke bila kuongea naye. So iwapo unataka mwanamke akunotice, wakati mwingine inahitajika kuwa na jitihada za ziada. Kukaa sehemu moja kungojea mwanamke akugundue haitakuwa ya fanaka kama vile ambavyo utaamka na kujifanya uonekane wewe mwenyewe.
So utafanyaje mpaka mwanamke akunotice? 

Tangamana na marafiki, jamiiana na kila mtu ambaye unamjua. Wakati umetoka matembezi au sehemu yako ya kujivinjari, ongea na kila mtu - wanaume, wanawake, wateja, wafanya kazi nk. Wanawake watauona uwezo wako wa kutangamana na kila mtu na watakuwa na interest ya kuongea na wewe. Ziada ni kuwa utakuwa unaonyesha ujiaminifu, urafiki, na uko na uwezo wa kujicontrol katika jamii - tabia zote ambazo wanawake wanaziona nzuri katika mwanaume. [Soma: Jinsi ya kupandisha hadhi yako kwa mwanamke]
7. Wafanye wanawake wakufukuzie
Kufanya wanawake wakufukuzie inaweza kuwa rahisi sana.  Kile ambacho unahitajika ni kutoka nje umakinike na kujifurahisha muda wote. Weka tabasamu katika uso wako na ujiinjoy wewe mwenyewe. Hii itamfanya mwanamke kukunotice na kutamani kuungana na wewe ili muinjoy pamoja.

Dalili 7 Za Kuonyesha Anakucheat Na Mwingine

Katika mahusiano huwa kuna changamoto tofauti tofauti. Kwa kawaida ni muhali kupata mahusiano ambayo hayana patashuka moja au nyingine. Inajulikana ya kuwa mahusiano huwa kuna migogoro, kutoelewana, kunyamaziana na mbaya zaidi...vita.

Anyway mambo kama haya huwezi kuyazuia kwa sababu wenyewe ndio wanayaita mapenzi. Utaskia mtu akilalamika kuwa amemiss kugombana ama kuteteshana na mpenzi wake, jambo ambalo huwa ni la kawaida.

Ok. tukija katika mada yetu ni kuwa nataka nikuulize maswali yafuatayo. Je hivi karibuni umeona kama mpenzi wako amekuwa mtu tofauti na ilivyo kawaida? Je mpenzi wako imekuwa muda mrefu tangu mfanye mambo yenu ya kawaida ambayo mlikuwa mkifanya? Je unamshuku kama amepata mwingine?



Kama majibu yako ni NDIO basi hili chapisho nimeliandika spesheli kwako na nataka umakinike kwa kusoma dalili zetu tulizoziandika na kama yote yanawiana na dhana yako basi ni wakati wa kumfungukia mpenzi wako na umwambie kweupe kuwa umechoshwa na tabia yake ya 'kutoka nje', na umuulize kama amechoshwa nawe ili ukate minyororo ya kuwa naye ili uwe huru.

Zama nami!

Dalili #7: Muda mwingi anajaribu kujirembua kuoneka vizuri

Kuvalia vizuri kila wakati si jambo baya la kufanya katika mahusiano, mwanzo wapenzi hupenda sana kuhakikisha ya kuwa wanampendeza mwenza wao.

Lakini, ukiona ya kuwa anamakinika zaidi na upande wa kujifanya aonekane mrembo, basi itakuwa anajaribu kumridhisha mtu mwingine kando na wewe. Kama umemgundua kuwa anajaribu kuvalia vizuri wakati anatembelea hizi sehemu basi weka ? katika mawazo yako: Kazini, supermarket, mkahawa, na hata gym! [Soma: Sifa za mwanamke mzuri]

Makinika: Zile sehemu zake za kawaida anazozienda kama amezijeuza kuwa fashion show itakuwa ni ishara ya kuwa anakucheat.

Dalili #6: Anakuwa msiri na simu yake, pakatalishi yake nk

Kila mtu ana haki ya kuwa na faragha yake. Mwanzo, watu wengi hawapendi faragha yao ishambuliwe na hata wapendwa wao. But ishu itakuja wakati ambapo anakuwa msiri kuhusu vitu vyake zaidi kuliko awali.

Hii inaweza kumaanisha kuwa kunakuwa na migogoro isioisha wakati ambapo umechukua kuangalia simu yake hadi ule wakati anaudhika wakati umeingia kwa chumba chake akiwa anatumia kompyuta yake. Ukiona mtu akianza kuwa msiri zaidi ni kuwa atakuwa anawasiliana na mchumba mwingine ambaye ako naye.

Dalili #5: Anapunguza hamu ya kufanya tendo la ndoa hadi kukataa asilani

Hata watu waseme nini, kufanya mapenzi ni sehemu muhimu inayohitajika katika mahusiano. Kama hamfanyi mapenzi, utajihisi ya kuwa unabezwa na kukatalika na mpenzi wako.

Wakati umri unaposongea, utagundua ya kuwa kiasi cha mapenzi mnachofanya huwa kinapungua. Hio ni kawaida, lakini kuna hatua nyingine neno 'ni kawaida' linaondolewa.

Kukataliwa katakata kufanya mapenzi ama kutoa visababu inaweza kumaanisha kwa njia rahisi kuwa hajiskii kufanya mapenzi na wewe. Wakati mtu anakucheat, huwa anapoteza ule muungano wa kihisia na wewe na atakuwa hana hamu ya kufanya mapenzi na wewe.[Soma: Aina za wanawake ambao wanasumbua katika mahusiano]

Dalili 4: Kuna yule mtu kilinge (mysterious)

Wale watu kilinge ndio unaopaswa kuwaogopa zaidi. Wanaume na wanawake kwa kawaida watakuwa na marafiki wa jinsia ile nyingine, lakini kama utamwona mpenzi wako haachi kuongea kuhusu huyo mtu basi kuna tatizo.

Hata kama nia yake ni nzuri, anaweza kuwa na kitu ambacho ni zaidi ya kuwa marafiki. Kama hatakuruhusu ukutane na huyu mtu kilinge ambaye amekuwa akipoteza muda wake mwingi naye, basi kunaweza kuwa na kitu ambacho ni zaidi ya kuchat pekee.

Dalili #3: Anazozana na wewe zaidi ya kawaida

Kukefyakefya na kukufananisha na wengine ni jambo lisilokubalika katika usuhiano. Wakati ambapo hii itatoka kuanzia mzaha hadi kuwa serious, ni ishara ya kuwa anakucheat.

Mara nyingi, mpenzi akikosana na mwenziwe hujaribu kujitenga na majibizano. Lakini ukiona ya kuwa kila wakati anagombana na wewe kwa sababu ya mahusiano yenu basi ni ishara ya kuwa kuna mwingine ambaye anamwonyesha mapenzi ya dhati...na si wewe [Soma: Mada ambazo hupaswi kuongea na mpenzi wako]
Dalili #2: Anakutenga wewe na marafiki zako wa karibu
Wapenzi wawili ambao wamekuwa pamoja kwa muda mrefu huwa wanagawa marafiki pamoja. Hawa ni wale ambao nyinyi wawili mnawaingiza katika maisha yenu kadri miaka inavyosonga. Wakati umeona kuwa mpenzi wako anapunguza muda wa kuwa na wewe na anachofanya ni kuwatenga watu hawa, kawaida huwa kuna mtu anahusika.
Anaweza kuwa hana moyo wa kukabiliana na marafiki wa karibu na kuwadanganya kuhusu furaha anayopata katika mahusiano yenu. Hii inaweza kutokea baada ya muda mrefu ama akajitenga ghafla.
Dalili #1: Analijeuza neno ''tu'' hadi ''ni'' polepole
Neno ''tu'' katika mahusiano ni takatifu. Huu ni ule wakati ambao mwanaume na mwanamke wamewekeza shina la kuwa pamoja. Wakati mwingi, sana sana wanawake ndio huwa wa kwanza wa kubadilisha neno ''ni'' hadi ''tu'' halafu mwanaume akalizoea.
Hivyo katika mahusiano ukiona mpenzi wako ameanza kurudia kutumia neno ''ni'' itakuwa anajaribu kukutenga katika maisha yake, anajaribu kukufuta katika picha yake.
Mwisho ni kuwa kudanganya katika mahusiano ni swala zito ambalo linaibua hisia nzito, lakini dalili za kucheat zinaweza kutatiza zaidi.
Kukataa kufanya mapenzi ama kujaribu kujirembua inaweza kusababishwa na misongo ama kutojiskia shangwe yeye mwenyewe. Kabla ya kumlaumu kuwa anafanya mabaya, hakikisha ya kuwa kuna ishu inayoendelea, ama inaweza kuwa wewe ndiwe chanzo cha kufanya mahusiano yenu yavunjike [Soma; Dalili za kuwa mpenzi wako amechoshwa na wewe]